HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 20, 2024

YANGA KUKABIDHIWA MWALI LUPASO

Na John Marwa

MABINGWA mara 30 wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL Young Africans SC watakabidhiwa Kombe lao la 30 katika Dimba la Benjamin Mkapa 'Lupaso' Mei 25 katika mchezo wao dhidi ya Tabora United.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ally Shaaban Kamwe mapema leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

Kamwe amesema ubingwa huo wa 30 watakabidhiwa tarehe hiyo kutokana na maombi yao kukubaliwa na Bodi ya Ligi Kuu ya kutaka kukabidhiwa ubingwa wao kabla ya mchezo wao wa mwisho wa msimu dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Mei 28.

"Tunaenda kukabidhiwa ubingwa wetu wa 30 Mei 25 katika mchezo wetu dhidi ya Tabora United. Tunawapongeza Bodi ya Ligi kwa kukubali ombi letu la kukabidhiwa ubingwa katika mchezo huo ambao pia utapigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

"Katika ubingwa huu kinachowauma watu sio tu sisi kutwaa ubingwa hapana bali ni kufikisha nyota tatu kwa maana kila ubingwa mara 10 ni nyota moja, ubingwa mara 30 ni nyota tatu na ndio Klabu pekee nchi hii kuwa na nyota tatu katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara." amesema Kamwe.

Hata hivyo kabla ya mchezo huo wa ubingwa kikosi cha Wananchi kitaondoka kesho kuelekea Dodoma kuwavaa Dodoma Jiji FC hapo Mei 22 katika Dimba la Jamhuri Dodoma.


No comments:

Post a Comment

Pages