HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 17, 2024

Akiba Benki yatoa elimu ya fedha kwa wadau

Na Mwandishi Wetu

Benki ya, Akiba imesema itaendelea kuunga mkono serikali kwa kutoa elimu ya fedha huku ikiboresha huduma zake nchi nzima ili kusaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuchochea  kukua kwa  uchumi wa Taifa.

Ameyasema hayo Juni 14 ,2024 Jijini  Dodoma  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba, Silvest Arumasi wakati wa kuhitimisha    mafunzo ya elimu ya fedha yaliyojumuisha viongozi wa benki hiyo ,watumishi kutoka Wizara , taasisi na ofisi mbalimbali za serikali  lengo likiwa ni kubadilishana ujuzi na kujenga mahusiano mazuri huku wakifahamiana na kuweka mikakati ya pamoja namna ya kuwahudumia watumishi wa Umma kwa weledi zaidi na  na kujibu maswali huku wakitatua kero zinazojitokeza kiutendaji.

Mkurugenzi Arumasi amebainisha kuwa benki hiyo itawaangalia wananchi wa Dodoma kwa upekee kutokana na fursa mpya zilizopo katika Jiji hilo kwani serikali  imekuwa ikiendeleza  kustawisha Makao makuu ya Nchi.

 Hata hivyo ametoa rai kwa wananchi  kujishughulisha na biashara na wanapokwama benki hiyo ipo tayarj  kutoa  mikopo kwa riba nafuu .

"Tunaahidi kuwa benki itaendelea kuunga mkono serikali kwa kuwasadia wananchi kuwapatia mikopo nafuuu  ili kuinua mitaji yao pia kupanua wigo wa huduma nchi nzima ili kufikia azma ya kutoa mchango mkubwa  wa kuwepo kwa huduma shirikishi za kifedha yaani financial inclusion" amesema Mkurugenzi Arumasi.


Naye Bi Upendo Makula,  Meneja wa Tawi la ACB - Dodoma  aliwashukuru washiriki wote kwa kuitikia mwito  kwa ujumla wao.

Aidha washiriki wote waliishukuru Benki ya Akiba kwa mada nzuri za semina hiyo na wameahidi kutumia elimu hiyo kama chachu katika utendaji wao wa kila siku kwani wamejengewa    msingi imara  wa uelewa wa maswala ya fedha.


No comments:

Post a Comment

Pages