Naibu Waziri Mkuu Dk. Doto Biteko (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Kilimo, Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Christopher Mwalugenge (wapili kushoto) alipotembelea Banda la benki ya NMB katika sherehe za ufungaji wa maonesho na mnada wa mifugo uliyofanyika katika Kata ya Ubena Zomozi wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Ushauri Kilimo wa Benki ya NMB, Isaac Masusu na wapili kulia na meneja Mwandamizi idara ya Bima wa Benki ya NMB, Catherine Joshua (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
NAIBU
Waziri Mkuu Dotto Biteko ametoa wito kwa Wadau wezeshi wa wafugaji
nchini kuendelea kutoa elimu na mikopo ili waweze kufuga kibiashara
wapate tija katika ufugaji wao.
Amewataka wadau wezeshi hao
kutoishia kwa wafugaji wa kibiashara bali wawafikie wafugaji wa
kienyeji ili na wao waweze kuwa wafugaji wenye tija nchini kwani hilo
ndilo lengo la serikali ya awamu ya sita ambayo inalenga kuwanyanyua
wafugaji.
Naibu Waziri Mkuu Biteko amesema hayo leo Juni 16
wakati akifunga maonesho hayo ya siku tatu ambayo yamefanyika Ubena
Zomozi ,Halmashauru ya Chalinze Mkoani Pwani.
Naibu Waziri Mkuu
amefunga monesho hayo akimwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amepata udhuru , hivyo natoa
wito huu kwa uongozi wa Benki zulizo toa udhamini huu ambazo ni Benki
ya Kibiashsra ya Kilimo TADB na NMB kundelea kutoa elimu kwa wafugaji
kwani wao wamekuwa wakichangia migogoro na wakulima kutokana na kwenda
kulisha mifugo yao kwenye mashamba.
"Halmashauri za wilaya nchini zitunze maeneo ambayo yalitengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo"
Serikali
itaendelea kuunga mkono maonesho ya Wafugaji wa Kibiashara nchini ili
waendeleze haya maonesho ambayo yanatoa elimu na kutoa Uhalisia wa
ufugaji wa kibiashara utakaoongeza tija kwa wafugaji na kupata soko
katika soko la kimataifa.
"Maonyesho haya muyapeleke katika ngazi
za Kanda ambako yatakutana walengwa ambao ni wafugaji wa kienyeji na
wawape elimu wabadilike na kufuga kibiashara".
"Wafugaji
wanapitia changamoto nyingi hivyo hivyo msichoke kuwapa elimu ya
ufugaji wa Kibiashara nina imani watabadilika taratibu na badaye nchi
itakuwa na wafugaji wenye mifugo yenye faida.
"Msiwasahau
wafugaji wanaofuga kienyeji na mwakani naomba baadhi wawepo kwenye
maonesho haya kwani watakapokuja watajifunza na kubadilika"amesema
Biteko.
Wakati huohuo amewaonya wafugaji kuacha migogoro na
wakulima na kuacha tabia ya kupitisha mifugo yao kwenye mashamba ya
wakulima huku akiwasisitiza elimu itumike pamoja na sheria katika
kumaliza migogoro hiyo.
"Hivi sasa dunia inakwenda kidigitali
hivyo hatakwa sisi ambao tulilelewa katika familia za wafugaji nawaasa
mbadilike msiwe kama wafugaji wa zamani ambao walikuwa wakifuga na
kulalia ngozi lakini wafugaji wa kisasa wanalalia magodoro hivyo nanyi
mbadilike sasa mfuge mifugo itakayowaletea tija acheni kufuga kizamani"
amesema Biteko.
Akiwa katika banda la Benki ya Maendeleo ya
kilimo nchini TADB akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa
TADB David Nghambi amesema kuwa Benki hiyo kipindi cha miaka mitatu
wametoa mikopo ya zaidi ya Bil.13, wamewawezesha wafugaji kibiashara
ili wawe na uhakika wa masoko kimataifa kwa kunenepa mifugo, pia wametoa
mikopo ya bilioni 47 kwa wafanyabishara wa maziwa.
Aidha
akikagua banda la NMB Mheshimiwa Biteko amezindua huduma ya Bima kwa
mifugo ambayo ni 20,000 kwa mwana na inatoa kinga dhidi ya vifo vya
mifugo vitanyotokana na radi, majeraha ya ndani na nje kwenye eneo la
usafiri, moto, dhoruba, kung'atwa na nyoka mafuriko, magonjwa ya asili
na yasiyodhibitika kwa mifugo.
No comments:
Post a Comment