Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amewataka Wadau wa
Sekta ya Uvuvi nchini kuhakikisha wanawapa kipaumbele wavuvi wadogo
kwani ndio wanaochangia takribani asilimia 95 ya uvuvi wote Tanzania.
Dkt.
Biteko ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa
Kwanza wa Wavuvi Wadogo Baranı Afrika sambamba na Maadhimisho ya miaka
10 ya mafanikio ya sekta ya uvuvi wenye lengo la kutathmini sekta ya
uvuvi ilipotoka, ilipo sasa na inapoelekea na kushirikisha wadau
mbalimbali,taasisi zinazowasaidia wavuvi wadogo zilizoko Afrika na
kwingineko duniani.
Amewataka
wadau wa sekta ya uvuvi barani Afrika kuhakikisha wanaifanyia kazi
sekta ya uvuvi ili kuhakikisha inachangia kwenye pato la Taifa kwa
kuhakikisha rasilimalizi za uvuvi zinalindwa.
“Nitoe
wito kwenu wadau wa sekta ya uvuvi nchini kuhakikisha mnawapa
kipaumbele wavuvi wadogo kwani ndio wanaochangia takribani asilimia 95
ya uvuvi wote Tanzania”, amesema Dkt.Biteko
Ameongeza
“Takwimu zinaonesha kuwa nchi Tanzania inazalisha wastani wa tanı
475,579 za samaki katı ya hızo tani 429,168 zinatokana na uvuvi katika
maji ya asılı na kuchangia kiasi cha shilingi trilioni 3.4 ambapo ni
karibu na asilimia1.9 kwa mwaka”.
Aidha,
amesema licha ya jitihada zinazochukuliwa kwenye sekta ya uvuvi
Tanzania Kama ilivyo kwa bara la Afrika bado inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi,ushirikishwaji
mdogo wa wadau katika usimamizi wa shughuli za uvuvi hususani wanawake
na vijana pamoja na upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya kuvunwa.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa ni heshima kwa
Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa kwanza Afrika wa Wavuvi Wadogo
ambao chimbulo lake ni Mkutano wa kuadhimisha Mwaka wa Kimataifa wa
Wavuvi Wadogo na Wafugaji Viumbe kwenye Maji (IYAFA) uliofanyika Rome
nchini Italia Machi, 2023.
Ameongeza
kuwa lengo la Mkutano huo wa Kwanza wa Wavuvi Wadogo Afrika ni kutoa
fursa kwa Wavuvi Wadogo kushiriki na kupaza sauti zao juu ya kuboresha
uvuvi mdogo ikiwa ni pamoja na kuwezesha ushirikishwaji wa wavuvi wadogo
kwenye michakato ya uundwaji na utekelezaji wa sera, sheria, kanuni,
mipango na mikakati yote inayohusu wavuvi wadogo.
“Ni
muhimu kusema kwamba uchaguzi wa Tanzania haukuwa kwa bahati, ila ni
kwa kutambua umuhimu wa uvuvi mdogo kwenye nchi yetu, na hatua ambazo
nchi imechukua katika kuandaa na kutekeleza Mpango wa Nchi wa
Utekelezaji wa Mwongozo wa Hiyari wa Uvuvi Mdogo”, amesema Mhe Ulega.
Amefafanua
kuwa Kauli mbiu ya Mkutano huo “Muongo mmoja wa Maendeleo: Kuongelea
baadaye ya Uvuvi Mdogo Endelevu “ ilichaguliwa kutokana na kusherekea
miaka kumi ya utekelezaji wa Mwongozo wa Hiyari wa Uvuvi Mdogo ili
kufikia uvuvi mdogo endelevu. Mkutano huu utafanya tathmini ya hali
halisi ya utekelezaji Mwongozo huo wa hiyari, sambamba na utekelezaji wa
muundo wa kisera na Mkakati wa Mageuzi ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji
Afrika.
“Tanzania
ilikuwa nchi ya kwanza Duniani kuandaa Mpango kazi wa kutekeleza
Mwongozo wa Hiyari wa wavuvi wadogo ambapo katika mkutano huu tutapata
fursa ya kueleza uzoefu wetu kwa nchi nyingine.” Amesisitiza Mhe. Ulega.
Waziri
wa Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi kutoka nchini Malawi, Mhe.
Dkt. Michael Bizwick Usi amesema kuwa kupitia mkutano huo nchi wanachama
wanapaswa kujadili masuala yanayohusu sekta ya uvuvi mdogo barani
Afrika na kuangalia namna bora ya kuboresha kutokana na changamoto
zilizopo.
Naibu
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),
Ang’ele Makombo N’tumba amesema kuwa kuna haja ya kuwasaidia wanawake
katika sekta ya wavuvi wadogo na kuwa SADC kwa kushirikiana na wadau
watasaidia nchi wanachama ili kuboresha sekta hiyo pamoja na kuzuia
uvuvi haramu.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), Dkt. Tipo Nyabenyi Tito
amesema licha ya kuwepo kwa changamoto zinazowakabili wavuvi wadogo
ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi na kuwa FAO itashirikiana na wadau wa
sekta ya wavuvi wadogo kwa kukuza uelewa na uwezo kwa wavuvi hao.
Kwa
upande wake, Rais wa Mtandao wa Wavuvi Wadogo Barani Afrika, Bw.
Gaoussou Gueye amesema kuwa sekta ya uvuvi mdogo ni muhimu hivyo
inatakiwa kutumia vifaa vya kisasa ili kuongeza tija ya shughuli za
uvuvi na kuwa wanawake wako katika sekta mbalimbali kuanzia ukusanyaji
wa samaki hadi kuuza kwa walaji.
“Kama
tunataka kusaidia uvuvi uwe endelevu lazima tuwe na mazingira wezeshi
kwa wanawake ili kuleta usalama wa chakula katika bara la Afrika na
utoshelevu wa chakula, katika uchumi wa buluu tunapaswa kulinda uchumi
wetu kwa kukuza sekta kwa maendeleo ya Afrika.” Amesema Gueye.
No comments:
Post a Comment