HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 08, 2024

INEC YAVIKABIDHI VYAMA VYA SIASA ORODHA YA VITUO VYA UBORESHAJI WAPIGA KURA


 
Na Mwandishi Wetu,
Wapiga kura 11,936 wanatarajiwa kupiga kura kesho tarehe 09 Juni, 2024 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo tarehe 07 Juni, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akisoma risala kwa ajili ya uchaguzi huo na kuongeza kwamba uchaguzi utahusisha vituo 29 vya kupigia kura.
 
“Jumla ya wapiga kura 11,936 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) watashiriki katika uchaguzi huu mdogo na jumla ya vituo 29 vya kupigia kura vitatumika,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Wagombea wanaowania Kiti cha Ubunge jimbo la Kwahani majina yao na vyama katika Mabano ni Bw.  Bashir Yatabu Said (Demokrasia Makaini), Bi. Nuru Abdulla Shamte (DP), Bi. Mwanakombo Hamad Hassan (NLD), Bi. Zainab Maulid Abdallah (CCK), Bi. Tatu Omary Mungi (UPDP), Bw. Khamis Yussuuf Mussa (CCM) na Bi. Jarade Ased Khamis (AAFP).
 
Wengine ni  Bw. Kombo Ali Juma (NRA), Bi. Shara Amran Khamis (ADC), Bi. Naima Salum Hamad (UDP), Bi. Madina Mwalim Hamad (ADA TADEA), Bw. Amour Haji Ali (SAU), Bi. Mashavu Alawi Haji (UMD) na Bw. Abdi Khamis Ramadhan (CUF).
 
Mwenyekiti wa Tume amevikumbusha vyama vya siasa, wagombea, mawakala wa vyama, wapiga kura na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kwamba hawapigi kampeni siku ya kupiga kura kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
 
 “Alama za vyama vya siasa zinazoashiria kampeni kama vile vipeperushi, bendera na mavazi haviruhusiwi kutumika kesho tarehe 08 Juni, 2024 ambayo ni siku ya uchaguzi,” amesema.
 
Jaji Mwambegele ameongeza kwamba zoezi la kupiga kura katika maeneo yote ya uchaguzi litafanyika katika vituo vilevile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
 
Ameongeza kwamba vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10:00) jioni.
 
“Iwapo, wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura katika mstari ambao wamefika kabla ya sa… WAPIGAKURA 11,936 KUPIGA KURA KWAHANI
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa), Jacobs Mwambegele akikabidhi nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura kwa viongozi na wawakilishi wa Vyama 19 vyenye usajili kamili wakati Vyama hivyo vilipokutana katika mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari.

Mapema wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Jaji Mwambegele aliahidi kuvipatia nakala hiyo vyama vyote na pia Vyama hivyo vitapatiwa nakala tepe ya orodha hiyo. 

“Leo kila chama kitapewa nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura. Dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha Kupanga na kuweka mawakala wa uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura,” amesema Jaji Mwambegele.

Vyama hivyo vilivyopokea ni AAFP, ACT - WAZALENDO, ADA - TADEA, ADC, CCK, CCM, CHADEMA, CHAUMA, CUF, Demokrasia Makaini, DP, NCCRA- MAGEUZI, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UMD na UPDP.


















No comments:

Post a Comment

Pages