HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2024

NHIF IKO KITAANI KWAKO MBAGALA WEMEITIKA

Kaimu Meneja wa NHIF Ofisi ya Mkoa wa Temeke, Canon Luvinga akiwahamasisha Wananchi kujiunga na bima ya afya kwenye wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya NHIF Kitaani Mwako katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. NHIF IKO KITAANI  KWAKO MBAGALA WEMEITIKA

Wananchi wakifuatilia.

Meneja wa NHIF Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Dkt. Raphael Mallaba (wapili kulia) akiwa na Meneja wa NHIF Ofisi ya Ilala Dkt. Aifena Mramba wakitoa elimu kwa wakaazi wa mtaa wa zakhem wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya NHIF KITAANI MWAKO iliyozinduliwa jana ktk viwanja vya Zakhem jijini dar es salaam jana. (Na Mpiga Picha Wetu).





Na Mwandishi Wetu

 

Wananchi tambueni  kuwa  kukata bima ya afya SI tu pale unapougua au ndugu anapougua ndiyo tufikirie kuja NHIF.. yamesemwa na kaimu meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Temeke, Canon Luvinga wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uhamasishaji Wananchi kujua faida na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya katka viwanja wa Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam
Huu ni mkakati endelevu  wa  kuwafikia Wananchi kwenye Kila tarafa za wilaya, kwani kuelimika ni jambo la kwanza na kufanya maamuzi ya kujiunga ni hatua nyingine, kwani tumebaini wananchi wengi Wana uelewa mdogo kuhusu bima ya afya. alisema.


Unakuta ndugu anakuja ofisini kuuliza gharama za kuliipia bima ya afya wakati huo huo anakwambia huyu ni mgonjwa na tumejipiga hata hivyo tunaenda kuuza kiwanja Ili tumkatie bima ya afya,hili nalo limetusukuma kutoka ndani ofisini na kuja kumuelimisha mwananchi asiingie kwenye umasikini kwa sababu ya maradhi hili hali bima ya afya ipo..alisema.

 
Ni mafanikio makubwa kwetu kupata idadi kubwa ya Wananchi waliojitokeza kushiriki uzinduzi wa kampeni hii kwani takribani watu 800 walihudhuria,mbali ya elimu pia huduma za upimaji  afya Bure kwenye magonjwa yasiyoambukiza zilitolewa na madaktari kutoka nhif ,ambapo watu 380 waliweza kupima afya zao kati yao 30 walibainika kuwa na dalili za magonjwa ya kisukari na presha hivyo walishauriwa kuhudhuria kwenye vituo vilivyo karibu kwa ufuataliliaji.


Hata hivyo watu 70 waliweza kusajiliwa papo kwa papo.alisema Kaimu Meneja. 


Tumedhamiria kama  ofisi ya Temeke ni kuhakikisha mwananchi anafahamu vyema faida na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kwani tumeona Kuna ombwe kubwa la uelewa kuhusu bima ya afya hivyo Mimi na timu yangu tumejipanga kutokukaa ofisini bali kwenda mtaani mwananchi aone ipo haja ya kujiunga na ukizingatia serikali inakuja na mpango wa bima ya afya kwa wote hii itasaidia kujenga uelewa zaidi.


Nao Wananchi walioshiriki wamekiri kuwa huu ni mpango mzuri kwani tulio wengi tunaona bima ya afya ni gharama kubwa lakini kwa elimu tuliyoipata kwanza tunaweza kubana vipato vyetu kwa kudunduliza na kuweza kulipia bima ya afya kwani tumeambiwa unalipa mara moja unapata huduma mwaka mzima.

No comments:

Post a Comment

Pages