HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 07, 2024

WAFANYABIASHARA KARIAKOO WAIOMBA SERIKALI TOZO ZOTE ZA MIZIGO KUISHIA BANDARINI

Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam

JUMUIYA  ya Wafanyabiashara Kariakoo wamemuomba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoa maelekezo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kushughulikia tozo zote mizigo ikiwa Bandarini kusaidia  kuondoa usumbufu bidhaa  zinapoongizwa sokoni.


Hayo yamebainishwa leo, Juni 7, 2024 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara, Martine Mbwana,  wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wamekuwa wakipata kero ikiwemo tozo za biashara zao  kutoka kwa baadhi taasisi za kiserikali wakati wengine kukutana na vishoka wanaojifanya watumishi wa Brela au TRA .

"Tunashukuru baadhi ya kero zilishughulikiwa na Waziri Mkuu kwa kutoa maelekezo kwa TRA  hivyo tunaomba pia  tunawaomba TRA wanapotekeleza majukumu yao wasijifiche,tushirikisha ,tufanye kazi kwa pamoja tujenge nchi yetu sote, wafanyabiashira tupo tayari kulipa kodi bila shuruti,  hata wanapoleta vijana wapya  kukusanya kodi watutambulishe wasijifiche wakawa wanawawinda wafanyabiashira"ameeleza Mbwana

 Hata hivyo amesema ni ukweli kuwa  wafanyabiashara wanamachungu ambayo hayana mfano na kimbilio lao  ni Rais  Dkt Samia  Suluhu Hassan kwani wanaamini ndio mtetezi wao katika jambo hilo, amesema.

Sanjari na hayo amefafanua  kuwa  kero kuna baadhi ya watu wakishirikiana watu kutoka taasisis za kiserikali  wanaolalamikiwa na wauzaji wa manukato( Pafyumu) wanaokwenda bandarini kuangalia mizigo inayoshuka kisha kukimbilia BRELA na kusajili haraka jina la bidhaa na  kushirikiana na baadhi ya watumishi wa serikali wakilalamika nembo ya bidhaa yao kutumika na kusababisha kukamatwa baadhi ya bidhaa na hao wafanyabiashara kupelekea kufilisika hivyo ni vyema suala hilo likafanyiwa uchunguzi ili ijukane bidhaa ikiingia kutoka nje na Kampuni inayoizalisha.

Pia amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele kikubwa kwa wafanyabiashira ambapo wamekutana na wizara zaidia ya tano ikiwemo wizara ya fedha na wizara mama ya viwanda na biashara na kufanyamazungumzo yanayochangia uboreshaji wa mazingira ya wafanyabiashara nchini.


Aidha amebainisha baadhi ya Kero zinazoendelea wakabili  wafanyabiashira hao kuwa ni pamoja na VAT,namna ya uwasilishaji wa risit za EFD, na uingizaji wa mizigo kutoka nje.

Aidha Jumuiya ya Wafanyabishara Kariakoo wanatarajia kufanya kufanya Mkutano June 11 ,2024 katika Ukumbi wa Anatoglo   na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila kuzungumza Mafanikio yao na kero zao zote kwa ujumla ili zipatiwe ufumbuzi hivyo Wafanyabiashara wanaalikwa kuhudhuri siku hiyo kuanzia asubuhi saa mbili

No comments:

Post a Comment

Pages