HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2024

YANGA HII TEMA MATE CHINI, YAISHANGAZA AZAM FC

Na John Richard Marwa

Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania klabu ya Young Africans wamefanikiwa kutetea ubingwa wao wa Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup baada ya kufanikiwa kapata mikwaju ya penati zaidi baada ya dakika 120 kumalizika kwa suluhu katika mchezo wa Fainali dhidi ya Azam FC.

Yanga sasa wanakuwa Mabingwa mara nne na kuwa vinara wa kombe hilo tangu kurejeshwa kwake msimu wa 2015/16 wakilitwaaa mara nne zaidi ya Watani zao Simba SC ambao wanawafuatia kwa kuchukua mara tatu huku Azam FC na Mtibwa Sugar wakiwa wametwaa mara moja moja kila timu.

Mchezo huo wa Fainali ulipigwa jana usiku katika Dimba la New Amani Complex Zanzibar na kushuhudiwa na mamilioni ya wapenda Soka ndani na nje ya nchi kupitia runinga, radio na miatandao ya kijamii.

Ulikuwa mchezo wenye hadhi ya Fainali kutokana upinzani ulioonyeshwa na timu zote mbili kuanzia dakika ya kwanza hadi kwenye mikwaju ya penati baada ya dakika za kawaida kukosekana kwa mshindi.

Azam walicheza vizuri sana kipindi cha kwanza licha ya kukosa umahiri wa kutengeneza nafasi lakini waliuchukua mchezo huku Yanga wakishambulia kwa kushitukiza kupitia kwenye nusu nafasi ambazo Azam walikuwa wakiziacha kwenye maeneo yao ya pembeni.

Kipindi cha pili Yanga walirejea kwa kishindo na kushinikiza mashambulizi langoni mwa Azam lakini uimara wa mlinda lango wa Azam Mohamed Mustafa alikuwa kizingiti kwa kuokoa mikwaju saba ya wazi kwenye dakika zote 120.

Dakika 90 za Mwamuzi Ahmed Arajiga zinatamatika Dimba la New Amani Complex hakuna mbabe, dakika 120 hakuna mbabe na mikwaju ya penati inaamua kwa Wananchi kutwaa taji hilo kwa penati 5-6.

Yanga wanatamatisha msimu kibabe kwa kufanikiwa kutetea mataji yao  mawili ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL na CRDB Federation Cup huku wakipokwa taji la ngao ya jamii na watani zao Simba SC.


No comments:

Post a Comment

Pages