HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 23, 2024

DC MAGOTI AAHIDI MAKUBWA BAADA YA KUKABIDHIWA GARI NA RC PWANI

NA VICTOR MASANGU, PWANI

Mkuu wa mkoa wa Pwani Alhaji  Abubakari Kunenge amekabidhi Magari mawili mapya  kwa wakuu wa Wilaya za Kisarawe na Bagamoyo ambayo yataweza  kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa kuwahudumia wananchi wao kwa urahisi zaidi.


Akikabidhi Magari hayo kwa wakuu hao wa Wilaya Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani amemshukuru kwa dhati  Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Magari hayo yatakayokuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la usafiiri kwa wakuu hao wa Wilaya.

Kunenge alisema kupatikana kwa magari hayo mapya kutaweza ni juhudi kubwa ambazo amezifanya Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anaboresha mazingira ya kazi kwa wakuu wake wa Wilaya.

Alisema katika Mkoa wa Pwani kuna jumla ya Wilaya sana na kwamba Rais kwa awamu hii ameshatoa magari mapya  matatu ambayo mawili yamekabidhiwa leo rasmi na mengine yatakabidhiwa katika awamu nyingine.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amempongeza kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa  kuwapatia magari hayo ambayo yatakwenda kuwa msaada mkubwa.

Magoti alisema kwamba hapo awali alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa kutumia gari nyingine lakini kwa sasa anashukuru kupata gari jipya ambalo litamuwezesha kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.

"Kwa kweli napenda kumshukuru kwa dhati Mkuu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Rais wangu Dkt.Samis Suluhu Hassan kwa kuweza kutupatia magari haya ambayo kwa kweli mimi nilikuwa naenda vijijini kwa usafiri wa gari aina ya Pick up, alisema Magoti.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  Halima Okash   hakusita kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kazi nzuri anayoifanya pamoja na Rais Samia  kuwapatia magari mapya kwa ajili ya kurahisisha usafiri na utekelezaji wa majukumu yao ya kuwatumikia wananchi

No comments:

Post a Comment

Pages