Na John Marwa
We huogopi? Eti huogopi Mnyama Simba kuanzia msimu mpya mbugani Mikumi kwa ajili ya uzinduzi wa kilele cha wiki ya Simba kuelekea Simba Day Agosti 3 katika Dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Klabu ya Simba kupitia Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema ufunguzi rasmi wa wiki ya Simba kuelekea kilele cha Tamasha kubwa la soka Barani Afrika utafanyika katika Mbuga ya Mikumi mkoani Morogoro huku safari ikianzia kwenye treni ya mwendo kasi ya SGR.
“Lengo la mkutano huu ni kutangaza rasmi kuanza kwa Wiki ya Simba 2024 pamoja na maandalizi yote kuelekea Siku ya Simba (Simba Day). Kama mnavyojua kila mwaka tunajaribu kufanya jambo jipya ili kuongeza thamani ya jambo letu.”
“Twendeni Hifadhi ya Mikumi tukawaonyeshe Watanznia kuna hifadhi, ni karibu na kiingilio ni 5,900. Kuna wengine wakisikia utalii wanajua ni mamilioni kumbe ni hela kidogo. Lakini pia ni kwenda kutangaza treni mpya ya SGR. Kwanza ni bidhaa mpya ambayo inatakiwa kutangazwa na sisi Simba Sports Club ndio Wenye Nchi kuitangaza.”
Ahmed ameongeza kuwa “Safari yetu itakuwa ni Julai 24, 2024 na treni itaondoka Dar es Salaam saa 12:00 alfajiri, muda wa kufika kituoni ni saa 11:00 alfajiri. Wale wote ambao wanatamani kuungana nasi kuelekea Morogoro kufika kwa wakati. Tutafika Morogoro saa 1:30 asubuhi. Mpaka sasa tumekodi behewa tatu kwa ajili ya Wanasimba na kwa mashabiki wetu hakutakuwa na nauli. Kila shabiki wa Simba ambaye anahitaji kuandika historia kupanda SGR, kufika Mikumi, kushiriki uzinduzi wa Wiki ya Simba afike akiwa na jezi ya Simba.”
Tukifika Morogoro tutakuta Wanasimba wenzetu wamekuja kutupokea. Kwa hili niyashukuru matawi ya Simba Morogoro. Tunataka kwenda kuishangaza Morogoro na ninyi mnatujua sisi sio watu wa kufanya mambo madogo madogo, tunafanya kwa ukubwa wake. Na nichukue nafasi hii kuwambia wakati wa Morogoro anayekwenda kazini awahi mapema kabla ya saa 1:30 asubuhi maana Mnyama akifika atakuwa mtaani kufanya hamasa zake.”
“Tutafanya utalii mbugani na baada ya hapo tutacheza mechi tutarudi Morogoro mjini na kuanza sfaari kurudi Dar es Salaam. Hii itakuwa tarehe 24, Julai. Tutakwenda na kurudi lakini kama ukitaka kulala Morogoro unaruhusiwa.”- Semaji Ahmed Ally.
No comments:
Post a Comment