HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 25, 2025

Moto wa Yanga waiunguza Pamba Jiji, Kouma afungua akaunti ‎

MABINGWA wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Yanga, wameuanza kwa kishindo msimu wa 2025/26, baada ya kuwachapa 'Wana TP Lindanda' Pamba Jiji ya Mwanza kwa mabao 3-0, pambano lililopigwa dimbani Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. 

‎Lassine Kouma ameweka rekodi ya kufunga bao la kwanza la Wana Jangwani hao wanaonokewa na Romain Folz, baada ya kuunganisha kimiani kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Edmund John mwishoni mwa dakika 45 za kwanza.

‎Katika kipindi cha pili, Yanga iliendelea kutawala mchezo na kufunga mabao mawili, moja la Maxi Nzengeli akiunganisha pasi ya Mohamed Hussein 'Tshabalala.'

‎Mtokea benchi Mudathir Yahaya Abbas alipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Pamba Jiji akifunga kwa kichwa akiitendea haki krosi maridhawa ya Pacome Zouzoua.





No comments:

Post a Comment

Pages