Na Mwandishi Wetu
WATOTO 103,668 wenye umri wa miaka mitatu mpaka 12 wamefikiwa na mradi wa ujifunzaji kwa mbinu ya michezo katika wilaya za Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma.
Mradi wa ujifunzaji kwa njia ya michezo 'Play Matters' umetekelezwa hapa nchini kwa miaka mitano ukilenga kuwafikia watoto 100,000 wanaoishi kwenye kambi za wakimbizi hapa nchini.
Akizungumza leo Septemba 24,2025 wakati wa kufungwa kwa mradi huo, Mkuu wa mradi wa Play Matters, Juliana Nyigura amesema mradi huo umevuka lengo na kuacha alama ya mafanikio katika sekta ya elimu hasa kwa kundi lengwa.
'PlayMatters umepata mafanikio kwa kuvuka lengo kwa kuwafikia watoto 3,668 zaidi walionufaika na mazingira ujifunzaji shirikishi, yanayofurahisha na salama huku walimu 1860 wakipata mafunzo ya ujifunzaji kwa mbinu ya michezo na kuboresha mbinu za ufundishaji sambamba na kuimarisha uhusiano wa walimu na wanafunzi.
"..Pia mradi uliwafikia viongozi wa kijamii 1,156 katika wilaya zote mbili kupitia hafua mbalimbali za kuwezesha ujifunzaji kwa mbinu ya michezo na wataalam 45 wanaoweza kufundisha mbinu bora na sahihi za ujifunzaji kupitia michezo kwa watoto wadogo," amesema Nyigura. 
Gervas Sembeye, Ofisa Elimu Mkoa wa Kigoma, amesema mradi wa Play Matters umeacha alama na kuahidi kuendelezwa katika wilaya zote nane za mkoa huo na kulishukuru Shirika la International Rescue Committee (IRC) wakishirikiana na Plan Tanzania waliotekekeza mradi huo wa miaka mitano.
"Tumeona ongezeko la ufaulu na uelewa kwa watoto wetu kipindi chote cha mradi, hakika mmeweza ninawaahidi Kigoma tutaienzi alama hii bora mliyotuachia," amesema Sembeye.
September 25, 2025
Home
Unlabelled
Play Matters yawafikia wanafunzi 103,668 kambi za wakimbizi
Play Matters yawafikia wanafunzi 103,668 kambi za wakimbizi
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment