HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 16, 2025

Jeshi la Polisi Dar lawashikilia Watuhumiwa 10 kwa kuendesha Televisheni Mtandao bila Leseni, Lawatoa hofu wananchi Uchaguzi Mkuu

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia Watu 10 kwa tuhuma ya kuenndesha Televisheni Mitandao bila ya kuwa na leseni. 

Akizungumza na wanahabari leo jijini humo Kamanda wa Kanda hiyo Jumanne Muliro amesema kuwa kati ya Oktoba 3 hadi 10 mwaka huu walfanikiwa kuwakamata watu wakiendesha televisheni hizo bila ya kuwa leseni za mamlaka husika huku akisisitiza ni kinyme na sheria ya uendeshaji wake.
" Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watu 10 wakiendesha televisheni mtandao bila ya leseni hii ni kinyume na sheria," amesema Kamanda Muliro.

Amewataja miongoni mwa watuhumiwa hao ni Japhet Lekingu, Joseph Augustino wote wa Wakazi wa Ukonga Sabasaba, Tegemea Mwinyigoha ( mkazi wa Tabata na Elias Pius makzi wa Mbezi Juu.

Amesisitiza kuwa watuhumiwa wamekutwa wakiendesha televisheni hizo bila ya kufuata sheria na kanuni za uendeshaji wake na kwamba watafikishwa mahakamani kwani upelelezi umekamilika.

Katika hatua nyingine, Kamanda Muliro Jiji la Dar es Salaam liko katika hali ya usalama huku akibainisha wananchi wanaendelea na shughuli zao kwa amani na utulivu.

Amefafanua kuwa wananchi wanashiriki kampeni za Wagombea wa Uchaguzi Mkuu kwa kusikiliza sera zao hivyo amewasisitiza wananchi kwenda kupiga kura Oktoba 29, 2025 ni haki yao ya Kikatiba.

No comments:

Post a Comment

Pages