Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema Mgombea wake wa nafasi ya Rais Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi yuko imara, akijiandaa kutwaa ushindi wa kidemokrasia ili kuiongoza tena Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kipindi cha pili.
Dkt. Mwinyi ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kufikia hatua hiyo anajivunia mafanikio aliyopata katika kutimiza kwa vitendo ahadi zake kwa wananchi na Ilani ya chama chake.
CCM, kimesema Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalenzo, Ismail Jussa Ladhu na chama chake hawana cha kuwaeleza wananchi kwani yote yametekelezxwa na Dkt. Mwinyi na kupitiliza.
" Jussa atabaki kuwa legelege na tepetepe kwakuwa hayo ndio maisha alioyachagua kuishi na wenzake" alisema Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, ameeleza hayo akijibu madai ya Jussa aliyedai kuwa Rais Dkt. Mwinyi yuko tepetepe kwa akihofia kushindwa Uchaguzi.
Mbeto alisema kwa haiba na ustawi wa mabadiliko ya maendeleo makubwa yaliochomoza chini ya uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi ni ujinga na upuuzi mtu kusema kiongozi huyo atashindwa uchaguzi .
Alisema siku zote wananchi wanahitaji kuona serikali yao ikiwatumikia kwa kuwaletea maendeleo ikiwemo kuimarika kwa huduma za kijamii na wananchi wakifaidika nazo .
Alisema Rais Dkt. Mwinyi yuko imara na madhubuti huku akisubiri siku ya kutangazwa na kuwa Rais kwa kipindi cha pili.
'Kwakuwa tumejiandaa kushinda lazima tuibuke na ushindi usio na longolongo. Sera za chama chetu zimejibu changamoto zote zilizokuwa zikiwatatiza wanchi katika sekta za Maendeleo. Tumetimiza ahadi na wajibu wetu. Ni haki yetu kupata ushindi wa kishindo" alisema Mbeto.
Katibu Mwenezi huyo aliongeza kusema mkataba wa miaka mitano iliopita kati ya wananchi na CCM ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi. Kazi hiyo kimsingi imefanyika kwa weledi na umakini mkubwa na kukamilika" alieleza
"Rais ametekeleza ahadi za kisera na zile zake binafsi hivyo hawezi kushindwa na mgombea anayetaka achaguliwe ili akafanye majaribio ya kuongoza nchi. Serikali si chumba cha maabara cha kufanyia majaribio" alisisitiza Mbeto.
Katibu huyo Mwenezi, amewahakikishiawananchi, wanachama wa CCM, wafuasi na Wakereketwa wake ,kujiandaa na kwenda kupig kura Oktoba 29 kisha wawe tayari kupokea matokeo ya ushindi.
"Jussa na wenzako jiandaeni kushuhudia kimbunga cha ushindi wa CCM kikiwapeperusha .na hila na njama zenu zimekwama hivyo jipangeni kutoka machozi bila kilio "alijinasibu Mwenezi huyo.



No comments:
Post a Comment