HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

March 13, 2026

CRDB yazindua Fainali Ndio Mpango na TemboCardVisa

Benki ya CRDB imezindua kampeni ya Fainali ndio mpango na Tembo Card Visa, kampeni ambayo inalenga kuhamasisha wadau, wananchi na wapenzi wa michezo kuhamasika kwenye matumizi ya kulipa kwa mtandao kupitia Tembo Card Visa  ambapo washindi wataweza kuhudhuria fainali za Kombe la Dunia nchini Marekani, Mexico na Canada.


Fainali hizo zitafanyika kuanzia mwezi Juni hadi Julai mwaka huu kwa Mataifa hayo matatu kuweza kushuhudiwa mataifa 48 yakimenyana kusaka ubingwa wa makala hayo ya 2026.



Akizungumza na Vyombo vya habari Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wa Kati CRDB, Bonaventure Paul, amesema kampeni hiyo ya Fainali ndio mpango na Tembo Card Visa, kwa sababu ni sehemu ya kuhamasisha Wananchi kutumia njia ya mtandao kufanya malipo kwenye manunuzi mbalimbali ya vitu na huduma.


"Kampeni hii ni sehemu ya jitihada ya Benki ya CRDB kuendelea kuhamasisha malipo ya kidijitali, kuleta ubunifu katika huduma za kifedha na kuwazawadia wateja wetu kwa uaminifu wake"


"Kama tunavyojua sote Mpira ni zaidi ya michezo, ni jambo linalounganisha watu duniani kote bila kujali Taifa, lugha na  tamaduni ambapo mwaka huu Dunia nzima itakusanyika kwa ajili ya kushuhudia mashindano makubwa ya Kombe la Dunia 2026, ambayo yataanza mwezi Juni mwaka huu."



"Na sisi kama CRDB tumeona nafasi ya kuwapa wateja wetu sehemu ya msisimko huo wa kimataifa. Kupitia kampeni hii wateja wetu watapata fursa ya kufurahia urahisi na usalama wa kutumia Tembo card visa huku wakipata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali za kuvutia na uzoefu wa kipekee, kampeni hii itaendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu, tumeizindua leo rasmi na itaenda hadi Juni 11mwaka huu,  ambapo itakuwa mwisho wa kampeni yetu kwa kuchezesha droo yetu ya mwisho." Ameongeza kuwa.


Katika kipindi hiki cha miezi mitatu wateja wanao tumia Tembo Card,  'Prepaid' Credit Card na Infinity Credit Card, yeyote anayetumia Card hizo ananafasi ya kushinda ambapo mteja atakayefanya miamala kuanzia 30 na kuendelea kwa kwa mwezi huyo atakuwa kwenye nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwa na lengo la kuhamasisha malipo yasiyotumia fedha taslimu  ambayo ni sehemu muhimu katika maendeleo ya sekta ya fedha nchini.




"Kiujumla tutakuwa na washindi 20, washindi 10 watajipatia zawadi ya wao kwenda kushuhudia mechi za Kombe la Dunia lakini washindi 10 watapewa zawadi za vifaa ambazo ni TV ya kisasa nchi 85, pamoja na kisimbuzi ili kuhakikisha huyu ambaye ameshindwa kwenda kufuatilia michuano hii mubashara basi akae nyumbani kwake kufuatilia michuano hiyo. 


"Washindi wa awamu ya kwanza watapatikana April 12, ambapo washindi wanne watajishindia nafasi ya kwenda Marekani kwa sababu ndiko itakapofanyika fainali. Lakini siku hiyo hiyo tutakuwa na washindi watatu wale ambao watajishindia Tv na Kisimbusi, droo ya pili itafanyika Mei 12 ambayo hii itakuwa na washindi watatu ambao watajishindia tripu ya kwenda Canada na washindi watatu ambao watapata Tv na Kisimbusi.


"Na droo yetu ya mwisho itakuwa Juni 11 ambapo itakuwa siku ya mwisho ya Kampeni yetu hii ambayo itachukua miezi mitatu, siku hiyo pia tutakuwa na washindi saba, watatu wataenda Canada na wanne watajishindia Tv na Kisimbusi." amesema Paul.


Kubwa zaidi kwa wateja na wapenda michezo ni kutumia fursa hiyo kuweza kushiriki matumizi ya kulipa kwa mtandao kupitia Tembo Card Visa kwa manunuzi kila siku ili kuweza kushinda miongoni mwa zawadi zilizowekwa mezani ikiwa ni kuhudhuria fainali za Kombe la Dunia na vifaa kama Tv na Kisimbusi.




No comments:

Post a Comment

Pages