HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

March 23, 2026

Ubora Unaoonekana; Benki ya NMB yan'gara tuzo za Euromoney 2026

Benki ya NMB imetwaa tuzo tatu katika Tuzo za Euromoney Private Banking 2026 jijini London, ikishinda Benki Bora ya Huduma za Wateja Maalum Tanzania, Benki Salama Zaidi ya Huduma za Wateja Maalum na Benki Bora kwa Uendelevu Tanzania.


Ushindi huo unazidi kuakisi uimara wa benki hiyo katika kutoa huduma mahususi kwa wateja, kuimarisha usalama wa fedha na kuongoza katika utekelezaji wa mikakati ya fedha endelevu. 


Mafanikio haya yanaendelea kuimarisha nafasi ya Benki ya NMB kama kinara wa ubunifu na mshirika wa maendeleo ya uchumi Tanzania na kanda ya Afrika Mashariki.


No comments:

Post a Comment

Pages