NA EDITHA WILLIAM, KAGERA
Hayo yamezungumzwa na Afisa Afya wa mazingira Manispaa ya Bukoba Jastin Samba wakati akiwa ofisin kwake ambapo amesema kuwa Mkoa wa kagera umepakana na na Nchi jirani ( Uganda, Rwanda, Burundi na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo) hivyo kuwataka wananchi kujiandaa kikamilifu kutokana na Nchi hizo kuwa tishio ya magonjwa ya milipuko
"Miaka ya nyuma tumeshuhudia ugonjwa wa Murburg ukitokea katika Mkoa wetu, lakin pia tulipata Tishio la pili ambalo lilitokea katika halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo." Amesema Samba
"Kwa mwaka juzi 2024 kuingia mwaka jana 2025 mwezi wa 12 mpaka mwezi wa kwanza kumekuwepo na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwahiyo Halmashauri ya Bukoba ipo katika hatari ya kupata magonjwa ya milipuko kulingana na muingiliano wa watu kutoka maneno mbali mbali."
Aidha, Samba amesema kwa sasa Kuna tishio la ugonjwa wa Ebola ambao umetokea Nchi ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ambapo ugonjwa huo pia umeathiri Nchi ya Uganda pamoja na Ufaransa, hivyo kuwata wananchi kuwa makini kutokana na muingiliano wa watu ulipo ili kuepukana na ugonjwa huo
Vile vile ameongeza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba imejipanga kikamilifu kuhakikisha inadhibiti magonjwa mlipuko kabla hayajatokea kwa kuchukua njia mbali mbali za kitahadhari ili kuweka jamii katika hali ya usalama ikiwemo njia za kitaalamu katika vituo vya kutolea huduma za afya
" Sisi kama Halmashauri kwanza tulifanya kikao Cha dharura kwa wataalamu wote wa huduma za afya pamoja na viongozi wote wanaosimamia maeneo yote ya kiutawala ili kuweka mipango mikakati namna gani tunaweza kunusuru hali hii ya ugonjwa wa Ebola "
Hata hivyo, kutokana na kuwepo kwa tishio la ugonjwa wa Ebola katika Nchi jirani, kwa Mkoa wa kagera na Nchi nzima ya Tanzania mpaka sasa hakuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola na hakuna mhisiwa yeyote wa ugonjwa huo
Sambamba na hayo, Samba ametoa rai kwa jamii kuzingatia njia za msingi za kuepuka magonjwa ya milipuko ikiwa ni pamoja kunawa mikono mara kwa mara, kutumia maji safi na salama, kula chakula kilichopikwa na kuiva vizuri, matumizi sahihi ya vyoo, kuzingatia usafi wa mazingira na kudhibiti wadudu wadhulifu.





No comments:
Post a Comment