Na Mwandishi Wetu, Singida
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu Stephen Wasira,
amewataka wanachama wa CCM kukutana mara kwa mara katika vikao rasmi vya
chama ili kujadili masuala muhimu na kuepuka kupotoswa na taarifa
zisizo na ukweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza
leo tarehe 19 Agosti, 2026 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wakati wa
kuanza ziara rasmi ya kikazi ya kukagua uhai wa chama, Wasira amesema
vikao hivyo vinawapa wanachama fursa ya kupata taarifa sahihi na
kuambizana ukweli.
"Wanachama wetu nchi nzima, kwa mujibu wa
Katiba mna vikao vya wanachama. Mkutane muambizane. Siku hizi kwenye
mitandao kuna uongo mwingi sana. Usipoangalia unaweza hata wewe
kushirikishwa kusema uongo," amesema.
Amesisitiza kuwa ni muhimu
wanachama kukutana na kujadili madai yanayosambaa, kisha kumtafuta mtu
mwenye ujuzi awasaidie kuyafafanua.
"Kwa hiyo ni vizuri kukutana
mkasema hili jambo limesemwa sana, maana yake ni nini? Mkamwita mtu
anayejua akawasaidia kufafanua," ameeleza.
Makamu Mwenyekiti huyo
amebainisha kuwa mikutano ya wanachama ni fursa muhimu ya kujadili
masuala yanayoendelea nchini ili waweze kukitetea chama ipasavyo.
Kuhusu uhuru na umoja wa nchi, Wasira amesema CCM itaendelea kulinda urithi huo uliopatikana kwa kazi kubwa.
"Hii
ndiyo CCM. Kazi ya kwanza tulipewa ni uhuru na tunalinda. Ya pili ni
umoja na tunahakikisha unabaki. Yeyote anayetaka kuubomoa anabomoa
msingi ambao hawezi. Anaweza kutikisa matawi lakini mizizi itabaki
chini," amesema.
Ameongeza kuwa wapo wanaodai CCM haijatekeleza chochote tangu uhuru, jambo ambalo amelisema ni kinyume na ukweli.
"Wanasema
hatujafanya chochote tangu uhuru. Lakini uhuru wa kusema ndio huo
walionao. Mdomo una kazi mbili: kusema na kula. Mtu akisema hakuna
chochote tangu uhuru, muache tu. Huyo ana matatizo anahitaji msaada,"
amehitimisha.
August 20, 2026
Home
Unlabelled
WASIRA ATAKA WANA CCM WAKUTANE, WASIINGIE MKENGE KWA MANENO YA MITANDAONI
WASIRA ATAKA WANA CCM WAKUTANE, WASIINGIE MKENGE KWA MANENO YA MITANDAONI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.





No comments:
Post a Comment