HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

August 20, 2026

Tuzo ya Mwalimu Nyerere Uandishi Bunifu imefika duniani

Na Mwandishi Wetu, Tanga


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda, amesema Tuzo ya Mwalimu Nyerere Uandishi Bunifu zinatambulika duniani.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa pazia la kupokea kazi bunifu kwaajili ya Tuzo za Mwalimu Nyerere Uandishi Bunifu leo Agosti 19,2026 amesema Dunia imetambua thamani ya Kiswahili na kuiheshimisha tuzo hiyo.



"Hili ni duru la tano, wakati tunaanza tuzo hii mwaka 2022/2023 tulianza na nyanja mbili ya Ushahiri na Riwaya ikaonekana kuwa ya kawaida lakini hapana tulipo sasa Dunia inajua ukiingia kwenye mitandao ukitafuta tuzo ya Mwalimu Nyerere unaiona... Hii ni heshima kwa taifa letu.


"...Tangu kuanzishwa kwa tuzo hii miswada 1,030 imewasilishwa kwa kamati huku nakala 292,000 za washindi wa kwanza wa tuzo hii zimechapishwa na kusambazwa kwa miaka minne," amesema Waziri Profesa Mkenda.


Waziri huyo amesisitiza kwamba malengo ya uanzishwaji wa tuzo hiyo ni kukuza kiswahili, kuhamasisha andishi, uchapaji, usambazaji, uuzaji na usomaji wa vitabu kwa lugha ya kiswahili.


Amesema malengo mengine ni kutambua, kutangaza na kuhifadhi tamaduni za taifa letu kwaajili ya vizazi vijavyo ndani na nje ya nchi.


"Washindi watatangazwa na kupewa zawadi zao Aprili 13,2027 siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere na kutaka washiriki wengi zaidi kuwasilisha kazi zao kwenye kamati kabla ya Desemba 30,2026," amesema Waziri Profesa Mkenda.



Waziri Profesa  Mkenda ameishukuru Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), kwa kuratibu tuzo hii chini ya Kamati ya Maandalizi inayoongozwa na Profesa Penina Mlama kwa mafanikio huku ikiongeza unaarufu ndani na nje ya nchi.


Akielezea mwenendo wa tuzo hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Ubunifu, Profesa Penina Mlama, amesema wanapokea kazi kutoka nyanja nne ambao ni Riwaya, Tamthilia, Ushahiri na Hadithi za Watoto.


No comments:

Post a Comment

Pages