Benki ya CRDB imesema zaidi ya wateja 700 wamepata zawadi kupitia droo mbalimbali za kampeni ya SimBanking, ikiwemo fedha taslimu kwa wafanyabiashara na kompyuta mpakato kwa wanafunzi.
Meneja wa Acquiring Business Benki ya CRDB, Hemed Kiluvia, amesema hayo wakati wa kuchezesha droo ya tatu ya mwaka na ya sita kwa mzunguko wa kila mwezi.
Amesema benki hiyo pia imeboresha huduma ya SimBanking kupitia mfumo unaoitwa “Mwaka wa Mbele,” wenye vipengele vinavyorahisisha huduma za kibenki.
Vipengele hivyo ni pamoja na kushiriki bili, kuchanganua na kuhakiki uhalali wa risiti, kuwezesha akaunti iliyolala na kutuma fedha kwa wateja walioko nje ya nchi.
Maboresho hayo yana lengo la kurahisisha huduma za kibenki na kuongeza usalama wa miamala kwa wateja.
#CRDBBank #SimBanking #HudumaKwaWateja #MwakaWaMbele #TeknolojiaYaKifedha




No comments:
Post a Comment