Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka,
akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), juu masuala mbalimbali yanayohusiana na
maendeleo ya mchezo huo, kwenye ukumbi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT),
jijini Dar es Salaam, juzi. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya RT, Tullo
Chambo na kushoto ni Mwanasheria wa shirikisho hilo, Thabity Bashiri. (Na Mpiga
Picha Wetu)
Na Elizabeth John
"Aidha, aliwashukuru baadhi ya wadhamini wanaoonesha
kuanza kuwaunga mkono, ukiwemo Mfuko wa Pensheni wa PPF, TSN Supermarket,
Symbion na S S Bakhresa".
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania , (RT), limetoa wito kwa
wadau mbalimbali nchini, kuunga mkono jitihada zao za kurejesha hadhi ya mchezo
huo nchini, kwa kudhamini matukio mbalimbali yakiwemo mashindano ya taifa yanayotarajia
kutimua vumbi, Agosti 23 na 24 mjini Morogoro.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rais wa
RT, Anthony Mtaka, alisema, mashindano hayo yamekuwa yakiendeshwa kwa hali
ngumu kutokana na kukosa wadhamini hivyo kuchangia kushusha hamasa na viwango
vya wanariadha.
Alisema, wanamichezo wasiopungua 450 kutoka
Tanzania Bara na Zanzibar, wanatarajia kushiriki mashindano hayo makubwa
kitaifa, ambayo yatasaidia kuibua vipaji vipya na kwamba, watakaofanya watapata
nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa, yakiwemo
yale ya vijana huko Mauritius Agosti 29 hadi 31.
Aidha, aliwashukuru baadhi ya wadhamini wanaoonesha
kuanza kuwaunga mkono, ukiwemo Mfuko wa Pensheni wa PPF, TSN Supermarket, Symbione
na S S Bakhresa.
Katika hatua nyingine, Rais huyo ametaka watu wanaopita
mitaani na kutumia mitandao kuichafua RT kutopewa nafasi na vyombo vya habari
kwani hawana nia nzuri na maendeleo ya mchezo huo.
Mtaka ambaye amerejea nchini hivi karibuni akitokea Moscow , Russia
katika mkutano mkuu wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF), ulioshirikisha
mataifa 206, alisema, moja ya mikakati ambayo ilizungumzwa kwenye mkutano huo
ni kuandaa wachezaji wenye ushindani katika mashindano makubwa, hususan
Olimpiki na Jumuiya ya Madola.
“Tanzania
inawakilishwa na wanariadha wawili katika mashindano ya Dunia ambayo
yanaendelea nchini humo, ambapo sisi kama
viongozi tumejipanga kupokea matokeo ya aina yoyote kutoka kwao, kutokana na
maandalizi wameyafanya,” alisema.
Wanariadha hao ni Msendeki Mohamed na Faustine Mussa
ambao leo wanatarajia kupeperusha bendera ya Tanzania katika mbio ndefu za km 42
(Full Marathon)
No comments:
Post a Comment