HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 19, 2014

Tanesco: Mgodi wa Kidatu bado una uwezo

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), limesema mgodi wa kufua umeme uliojengwa Kidatu Morogoro mwaka 1975, bado una uwezo wa kuzalisha nishati hiyo kwa kiwango cha kutosha.

Kauli hiyo, ilitolewa juzi na Meneja wa Mgodi huo, Injinia Joseph Lyaruu, wakati wa ziara ya wandishi wa habari nchini, kujionea kazi zinavyofanyika katika mgodi huo.

Alisema uwezo huo ulitokana na jitihada za Tanesco kuendelea kuuboresha hatua kwa hatua, ambako hivi sasa katika mgodi huo kumefugwa mashine nne ikilinganishwa na awamu ya kwanza ulipojengwa, ambazo zina uwezo wa kuzalisha umema kwa ufanisi mkubwa ambao unakwenda sambamba na ongezeko la wateja kila mwaka.

“Sio kweli kama mtambo hauwezi kuzalisha umeme kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu, bado unao uwezo wa kufanya kazi katika kipindi cha miaka 50, hata nchini India iko mitambo ambayo imefanya kazi zaidi ya miaka 50,” alisema Injinia Lyaruu.

Lyaruu, alisema Watanzania hawana haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu uzalishaji katika mgodi huo, kwa sababu shirika kwa kushirikiana na wahisani wako katika mkakati kubadili baadhi ya vifaa ambavyo vimekuwepo tangu unajengwa.

Akizungumzia kuhusu hali ya maji, Lyaruu alisema Watanzania watarajie kupata huduma hiyo kwa ufanisi na bila kikomo, kwa sababu kipindi hiki maji ya kutosha yapo.

Alizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni uhaba wa maji, shughuli za kibinadamu karibu na mito inayoingia kwenye mabwawa na uchepushaji wa maji kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu, Rashid Msingwa, alisema mgodi huo una wafanyakazi 104, ambao wanafanya kazi mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za jamii.

No comments:

Post a Comment

Pages