SHIRIKA la Ugavi wa Umeme
nchini (Tanesco), limesema mgodi wa kufua umeme uliojengwa Kidatu Morogoro
mwaka 1975, bado una uwezo wa kuzalisha nishati hiyo kwa kiwango cha kutosha.
Kauli hiyo, ilitolewa juzi na
Meneja wa Mgodi huo, Injinia Joseph Lyaruu, wakati wa ziara ya wandishi wa
habari nchini, kujionea kazi zinavyofanyika katika mgodi huo.
Alisema uwezo huo ulitokana
na jitihada za Tanesco kuendelea kuuboresha hatua kwa hatua, ambako hivi sasa
katika mgodi huo kumefugwa mashine nne ikilinganishwa na awamu ya kwanza
ulipojengwa, ambazo zina uwezo wa kuzalisha umema kwa ufanisi mkubwa ambao
unakwenda sambamba na ongezeko la wateja kila mwaka.
“Sio kweli kama mtambo
hauwezi kuzalisha umeme kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu, bado unao uwezo
wa kufanya kazi katika kipindi cha miaka 50, hata nchini India iko
mitambo ambayo imefanya kazi zaidi ya miaka 50,” alisema Injinia Lyaruu.
Lyaruu, alisema Watanzania
hawana haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu uzalishaji katika mgodi huo, kwa sababu
shirika kwa kushirikiana na wahisani wako katika mkakati kubadili baadhi ya
vifaa ambavyo vimekuwepo tangu unajengwa.
Akizungumzia kuhusu hali ya
maji, Lyaruu alisema Watanzania watarajie kupata huduma hiyo kwa ufanisi na
bila kikomo, kwa sababu kipindi hiki maji ya kutosha yapo.
Alizitaja baadhi ya
changamoto zinazowakabili kuwa ni uhaba wa maji, shughuli za kibinadamu karibu
na mito inayoingia
kwenye mabwawa na uchepushaji wa maji kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine.
Naye Mkuu wa Kitengo cha
Rasilimali watu, Rashid Msingwa, alisema mgodi huo una wafanyakazi 104, ambao
wanafanya kazi mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za jamii.
No comments:
Post a Comment