Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga (kulia), akipokea hundi ya sh. milioni 423.5 kutoka Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington kwa ajili ya klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Soka Tanzania.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
KAMPUNI ya Azam Media Ltd
inayomiliki Haki za Matangazo ya Televisheni kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL), jana imeikabidhi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board),
kiasi cha shilingi milioni 423.5 ambazo ni za awamu ya pili ya msimu huu wa
2014/15.
Makabidhiano hayo yalifanyika
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Golden Jubilee jijini Dar es Salaam,
ambapo kila klabu ya Ligi Kuu imeingiziwa katika akaunti yake mgawo wa shilingi
milioni 27.5, kwa ajili ya kusaidia maandalizi ya mwisho na masuala tofauti ya
ushiriki.
Akizungumza katika hafla ya
makabidhiano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPL Board, Silas Mwakibinga,
alizitaka klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom kuhakikisha inazitumia pesa hizo
kwa malengo yaliyokusudiwa, ili kuimarisha ushindani katika na kukuza kiwango
cha kila timu.
Azam Media Ltd inayomiliki kituo
cha televisheni cha Azam Tv, ilitangazwa mshindi wa zabuni za haki ya matangazo
ya televisheni kwa mechi za VPL, ambako katika awamu ya kwanza ya pesa hiyo
msimu huu iliyotoka Juni 1, mwaka huu, TPL Board ilipokea kitita cha shilingi
mil. 462, ambako kila klabu ilijibebea kiasi cha shilingi mil. 25.
Kwa mujibu wa Mwakibinga,
tofauti na msimu uliopita, ambako kila klabu ilipata kitita cha shilingi mil.
100 zilizotolewa katika awamu nne, msimu huu kila klabu itajinyakulia kitita
cha shilingi milioni 110, kwa awamu zote nne (sawa na shilingi milioni 27.5
kila awamu).
Kwa upande wake, Mtedaji
Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alizitakia kila la kheri klabu shiriki
katika Ligi Kuu na kwamba kituo chake kiko katika maboresho makubwa ya
muonekano wa mechi zitakazorushwa na Azam Tv One na Azam Tv Two, zikiwamo mechi
za usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
No comments:
Post a Comment