HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 21, 2014

CCM WAMUAGA AMINA IMBO

 Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria sherehe ya kumuuaga amina imbo.
  Na Fredy Mgunda, Iringa
Aliyekuwa Katibu wa chama cha mapinduzi  wilaya ya iringa vijijini AMINA IMBO ameagwa rasmi   kutokana na uhamisho aliopewa na chama hicho.

Akizungumza katika hafra ya kumuaga AMINA IMBO amewapongeza  viongozi wa chama hicho kwa kuwa  walikuwa wa wakimfundisha mambo mbalimbali ambayo yalikuwa yakilenga kukijenga chama hicho.

Amesema kuwa kutokana na mambo mengi aliyojifunza kupitia viongozi hao yamemsaidia kuwa jasili katika kazi yake na hata   kumsaidia kufanya vizuri katika uchaguzi  wa serikali za mitaa katika wilaya ya iringa vijijini.

IMBO pia amewashushia lawama viongozi wakubwa wa chama hicho mkoani iringa akiwemo mwenyekiti wa chama mkoa,katibu mwenezi wa iringa vijijini pamoja na mwenyekiti wa chama hicho wa wilaya ya iringa vijijini kwa kitendo cha kumchafua kwa njia ya simu ,maandishi kwa kutuma barua makao makuu ya chama bila kuwa na utafiti wowote kwa  mambo waliyoyaongea na kuyatenda hayakuwa na  ukweli wowote.

Hata hivyo ametoa  shukrani kwa mbunge wa jimbo la isimani WILIAM LUKUVI kwa kumsaidia  kufanya kazi na kuchangia kazi yake ionekane kwa umma na kumuongezea uwezo wa kuwa kiongozi mzuri ambaye ataendelea kuwa kioo cha jamii.


Naye katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya mufindi MIRAJI MTATURU amewataka viongozi wanaovamia siasa kufuata misingi yote ya siasa na kuacha majungu huku kwa kuwa bado hawajui siasa na wanaojua siasa ni wale watendaji  na kumpongeza AMINA IMBO kwa kufanya kazi nzuri kwa muda mfupi aliokuwepo katika wilaya hiyo.


Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa HASSANI MTENGA  amesema kunahaja ya chama hicho kurudi kwenye mstari kutokana na migogoro inayoendelea kwenye chama hicho kwa kuwa mambo yanaendelea yanaumiza na yanakuchangia kubomoa chama.

MTENGA pia amewataka  watendaji kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuwa chama hicho saizi kimevamiwa na watu wasio na taaluma ya siasa na kusababisha chama hicho kusambaratika kutoka na uchu wa madaraka wao,hivyo makatibu wanatakiwa kuwa makini.
Aidha amewapongeza makatibu wote wa wilaya ya iringa kwam kazi nzuri waliyoifanya katika uchaguzi wa serikali za mitaa huku akiwataka kufahamu kuwa uongozi si fedha bali ni kujua maadili yanayoendana na uongozi.


Mbali na hayo amemuonya katibu msaidizi wa iringa vijijini na kumtaka kujibadilisha na mwenendo alionao sasa na kujitaidi kuwa karibu na katibu anaetarajiwa kuja na kama kunatatizo lolote wanapaswa kufikisha katika ofisi ya katibu mkoa ili kuyamaliza na kuondokana na yaliyotokea kwa sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages