Na Fredy Mgunda, Iringa
Aliyekuwa Katibu
wa chama cha mapinduzi wilaya ya iringa
vijijini AMINA IMBO ameagwa rasmi
kutokana na uhamisho aliopewa na chama hicho.
Akizungumza katika
hafra ya kumuaga AMINA IMBO amewapongeza viongozi wa chama hicho kwa kuwa walikuwa wa wakimfundisha mambo mbalimbali
ambayo yalikuwa yakilenga kukijenga chama hicho.
Amesema kuwa
kutokana na mambo mengi aliyojifunza kupitia viongozi hao yamemsaidia kuwa jasili
katika kazi yake na hata kumsaidia kufanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika wilaya ya iringa
vijijini.
IMBO pia amewashushia
lawama viongozi wakubwa wa chama hicho mkoani iringa akiwemo mwenyekiti wa
chama mkoa,katibu mwenezi wa iringa vijijini pamoja na mwenyekiti wa chama
hicho wa wilaya ya iringa vijijini kwa kitendo cha kumchafua kwa njia ya simu
,maandishi kwa kutuma barua makao makuu ya chama bila kuwa na utafiti wowote
kwa mambo waliyoyaongea na kuyatenda
hayakuwa na ukweli wowote.
Hata hivyo
ametoa shukrani kwa mbunge wa jimbo la
isimani WILIAM LUKUVI kwa kumsaidia kufanya kazi na kuchangia kazi yake ionekane
kwa umma na kumuongezea uwezo wa kuwa kiongozi mzuri ambaye ataendelea kuwa
kioo cha jamii.
Naye katibu
wa chama cha mapinduzi wilaya ya mufindi MIRAJI MTATURU amewataka viongozi
wanaovamia siasa kufuata misingi yote ya siasa na kuacha majungu huku kwa kuwa
bado hawajui siasa na wanaojua siasa ni wale watendaji na kumpongeza AMINA IMBO kwa kufanya kazi
nzuri kwa muda mfupi aliokuwepo katika wilaya hiyo.
Kwa upande
wake katibu wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa HASSANI MTENGA amesema kunahaja ya chama hicho kurudi kwenye
mstari kutokana na migogoro inayoendelea kwenye chama hicho kwa kuwa mambo
yanaendelea yanaumiza na yanakuchangia kubomoa chama.
MTENGA pia
amewataka watendaji kufanya kazi kwa
uadilifu kwa kuwa chama hicho saizi kimevamiwa na watu wasio na taaluma ya
siasa na kusababisha chama hicho kusambaratika kutoka na uchu wa madaraka
wao,hivyo makatibu wanatakiwa kuwa makini.
Aidha amewapongeza
makatibu wote wa wilaya ya iringa kwam kazi nzuri waliyoifanya katika uchaguzi
wa serikali za mitaa huku akiwataka kufahamu kuwa uongozi si fedha bali ni
kujua maadili yanayoendana na uongozi.
Mbali na
hayo amemuonya katibu msaidizi wa iringa vijijini na kumtaka kujibadilisha na
mwenendo alionao sasa na kujitaidi kuwa karibu na katibu anaetarajiwa kuja na
kama kunatatizo lolote wanapaswa kufikisha katika ofisi ya katibu mkoa ili
kuyamaliza na kuondokana na yaliyotokea kwa sasa.
No comments:
Post a Comment