HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 06, 2017

WAAJIRI NA WAAJIRIWA ZINGATIENI SHERIA ZA KAZI KUONDOA MIGOGORO KAZINI: MAJALIWA

Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa waajiri na waajiriwa wote nchini kuzingatia Sheria za kazi na kuimarisha uhusiano katika kazi ili kutumia muda mwingi kufanya kazi badala ya kutatua migogoro kazini.


Ameyasema hayo alipokuwa akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.

“Niwaombe waajiri na waajiriwa kuzingatia Sheria za kazi tupunguze migogoro kazini ili tuweze kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufanya kazi” alisisitiza Mhe. Majaliwa.

Ameongeza kuwa Serikali imefanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 58 ya migogoro ya kikazi inatokana na kutozingatiwa kwa taratibu za kuachishwa kazi kwa waajiriwa.

Amezitaja Sekta zinazoongoza kwa migogoro ya kazi kuwa ni Usafirishaji,ujenzi,ulinzi,binafsi,elimu,huduma za Hotel na Viwanda.

Katika kupunguza migogoro mahali pa kazi Serikali imefanya kaguzi na kusimamia uundwaji wa Mabaraza ya Wafanyakazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi imeendelea kutimiza wajibu wake wa kusuluhisha migogoro ambapo katika kipindi cha Julai  hadi Februari  2016 jumla ya migogoro 8,832 ilisajiliwa na kati ya hiyo migogoro 3,319 sawa na asilimia 37.6 ya migogoro iliyosajiliwa imesuluhishwa.

No comments:

Post a Comment

Pages