HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2018

Tigo, Uber waingia makubaliano

NA SULEIMAN MSUYA

KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania na Kampuni ya Kiteknolojia Uber zimeingia makubaliano ambayo yatasaidia watumiaji wa usafiri Uber kupata usafiri huo bila kuwa kifurushi cha mtandao maarufu (bado).

Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakurugenzi wa kampuni hizo waliweka bayana kuwa makubaliono hayo yana faida kwa pande zote mbili.

Mkurugenzi wa Tigo Tanzania, Simon Karikari alisema kampuni yao ni moja ya kampuni yenye nembo kubwa nchini hivyo ubia huo walioingia na Uber utazidi kupanua wigo wao wa kibiashara.

Karikari alisema wateja wa tigo watapata huduma hiyo bila ya kuwa na kifurushi cha mtandao jambo ambalo litaongeza wateja wa usafiri wa Uber.

"Uber  ni kampuni ya Kimataifa hivyo ubia huu ni ishara tosha kuwa Tigo inakubalika na sisi hatutawaangusha kwani tumeshika asilimia kubwa ya soko la biashara ya mawasiliano ya simu nchini," alisema.

Alisema kwa sasa Tigo ina zaidi ya wateja milioni 11.3 hivyo ni matumaini yao kuwa ubia huo na Uber utachochea ongezeko kubwa la wateja kwa muda mfupi na pande zote kunufaika.

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo alisema ubia huo ni muhimu kwao na wateja wao kwa kuwa watapatikana bila gharama.

Msemo alisema madereva na wateja ambao wanatumia mtandao wa Tigo watakuwa wanawasiliana popote bila gharama jambo ambalo awali iilikuwa changamoto.

Alisema usafiri wa Uber umefanikiwa kutoa ajira zaidi ya 3000 na kuhudumia watu zaidi ya 200,000 kwa mwezi hivyo ubia huo utaongeza watumiaji wengi.

Meneja huyo alisema mikakati yao ni kuhakikisha kila mkazi wa jiji la Dar es Salaam anaweka kipaumbele katika kutumia Uber kama njia ya usafiri wa haraka kufika anapotaka.

"Tumekuwepo Tanzania takribani miaka miwili sasa kwa mafanikio makubwa lakini hatua ya leo kuingia ubia na Tigo ni hatua kubwa zaidi kibiashara naamini wateja wataongezeka maradufu," alisema.

Msemo alisema matarajio yao ni kuhakikisha wanafukia mikoa mingine kwa siku za karibuni ili kusambaza huduma hiyo.

Alisema kwa miaka miwili huduma ya Uber Tanzania imefanikiwa kuhudumia wageni kutoka nchi 70 duniani ambao wa wana App yao.

No comments:

Post a Comment

Pages