Na Elizabeth John
BAADA ya
kutamba na ngoma yake ya ‘Twende na mimi’, msanii wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Abrahaman Kassembe ‘Dullayo’, yupo katika
hatua za mwisho za uaandaaji wa kibao chake kipya baada ya kuwa kimya kwa muda
mrefu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dullayo alisema wimbo huo unaitwa ‘Nimeamua’ tayari umekamilika na
utaanza kusikika hivi karibuni katika vituo mbalimbali vya redio huku akiwa
katika matayarisho ya video ya kazi hiyo.
“Daa..! Hiyo ngoma itakuwa kali
kupita maelezo kutokana na kuandaliwa vyema kwenye studio ya Imotion, chini ya
mtayarishaji mahiri, Kisaka, ambaye namuamini na ninauhakika kautendea haki,” alisema
Dullayo.
licha ya kutoka na kibao hicho, Dullayo aliweza kutamba na vibao vyake kama vile Mida Ya Kazi, Naumia Roho na nyinginezo ambazo bado zinafanya vizuri na mashabiki kuziomba katika vipindi mbalimbali vya redio na televisheni.
Dullayo amewatuliza mashabiki wake kuwa bado ana kazi nzuri na za kuburudisha wanazotakiwa kuzisikia kutoka kwake, hivyo waendelee kumpa sapoti katika kile anachokifanya.
No comments:
Post a Comment