Na Elizabeth John
MKURUGENZI
wa Ufundi Wilaya ya Temeke, Kennedy Mwaisabula ‘Mzazi’ amewataka wahitimu wa
kidato cha nne kujitokeza katika kozi ya waamuzi kwa lengo la kuongeza ajira
kwa vijana.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mzazi alisema vijana waliomaliza
kidato cha nne wanaosubili matokeo wanatakiwa wajitokeze katika wilaya ya
Temeke kwaajili ya kozi hiyo ya muda wa siku saba na ada yake ni sh 45,000.
Alisema
darasa litaanza baada ya wao kujitokeza hadi kufikia 25 na kwamba hiyo ni ajira
kwa vijana ambapo watapata nafasi ya kufundisha ligi daraja la nne Wilaya ya
Temeke.
“Tumeamua
kufanya hivyo kwa kuona vijana wengi baada ya kumaliza kidato cha nne wanakuwa
mtaani, naamini hii itapunguza idadi hiyo tunaomba vijana wajitokeze kwa wingi ili
kuongeza idadi ya waamuzi katika soka letu,” alisema Mzazi.
Aliongeza
kuwa mbali na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne pia wanakaribishwa na vijana
ambao hawana ajira ili kuwanusuru vijana wanaoingia katika makundi yasiyofaa na
uvutaji bangi kwa kukosa ajira.
No comments:
Post a Comment