"Sina wasiwasi kuhusu kazi yangu wakati
wowote na kamwe sitojiuzulu kutokana na hili. Mimi sio mtoto mdogo. Najua
kuhesabu matokeo. Kama mchezaji anaonesha hayuko tayari kuendelea kutumika,
mimi lazima nioneshe utii kwa kutoendelea kumtumia"
MRENO
anayeinoa Real Madrid Jose Mourinho mwishoni mwa wiki amesisitiza kutokuwa na
mpango wa kujiuzulu nafasi yake katika klabu hiyo, licha ya kukubali kipigo cha
mabao 3-2 kutoka kwa Malaga
– kilichowaacha nyuma kwa pointi 16 dhidi ya vinara FC Barcelona.
Machungu ya
kichapo hicho kwa Mourinho ulichangiwa na uamuzi wake wa kumtema kikosini
nahodha na mlinda mlango wake namba moja Iker Casillas, ambaye mara kadhaa
ameripotiwa kuwa na mzozo nayem huku Special One akipinga hilo.
Mourinho
alionesha ukaidi wa kutojutia uamuzi wake wakati alipoulizwa kama
anahisi kibarua chake kimashakani kutokana na matokeo hayo samba na uamuzi wa
‘kumkaanga’ Casillas benchi.
"Sio
wakati wote, sina wasiwasi kuhusu kazi yangu wakati wowote na kamwe sitojiuzulu
kutokana na hili," alisema kocha huyo mropokaji anayetaka sasa aitwe ‘The
Only One badala ya Special One.’
"Mimi
sio mtoto mdogo. Najua kuhesabu matokeo. Kama
mchezaji anaonesha hayuko tayari kuendelea kutumika, mimi lazima nioneshe utii
kwa kutoendelea kumfanya hivyo."
Hii ilikuwa
ni mechi ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 kwa mshindi huyo wa Kombe la
Dunia akiwa na Hispania kutupwa benchi na mlinda mlango mwenye miaka 25,
Antonio Adan alipangwa katika pambano hilo
na kujikuta akimwangusha Mourinho.
"Kwa
sasa, kwangu mimi na benchi zima la ufundi, Adan ni mlinda mlango bora kuliko
Iker," alisema Mourinho.
"Tumekuwa
tukiumiza na kutugharimu kupitia idara kadhaa za kikosi chetu, mojawapo ni ya
ulinzi. Kocha anaaglia na kujikusanyia takwimu binafsi kujua nani yu bora
kucheza na kisha kumpanga na ndivyo nilivyofanya.
"Nyinyi
(vyombo vya habari) mnaweza kujua nini
mnahitaji lakini sio katika mambo ya kiufundi," alisema kocha huyo
akionekana kufura kwa hasira.
No comments:
Post a Comment