“Haikufikiriwa kwa mfano kwamba Chelsea
ingemudu kutwaa ubingwa wa Ulaya msimu uliopita, hasa baada ya kufanyika kwa
mabadiliko ya dawati la ufundi katikati ya msimu, lakini wakafanya hivyo. Tena
ikazichapa Barcelona
na kisha Bayern Munich katika fainali”
KOCHA wa
England Roy Hodgson amedai ni jambo ‘lisilowezekana’ kusema kikosi chake
hakiwezi kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia katika fainali zijazo nchini Brazil mwaka
2014.
Bosi huyo wa
‘The Three Lions’ amesema hayo akitumia matokeo ya Chelsea
kutwaa ubingwa wa Ulaya msimu uliopita baada ya kuzichapa Barcelona na baadaye Bayern Munich kwa
mikwaju ya penati kwenye dimba la Allianz Arena.
Hodgson
alisema: “Unaweza kusema kwamba tuko mbali mno na timu zinazopewa nafasi ya
kutwaa ubingwa wa dunia, hivyo kushinda kuwa ni jambo lisilo na uwezekano wa
kutokea.
“Lakini
unapaswa kuachana na hisia kwamba ’haiwezekani’ hasa katika soka.
“Kuna
matukio mengi mno katika soka unayoweza kuyachuklulia kama mfano hai juu ya hilo , kwamba unaweza
kusema haiwezekani, lakini mwisho wa siku watu wakafanya hivyo.
“Haikufikiriwa
kwa mfano kwamba Chelsea
ingemudu kutwaa ubingwa wa Ulaya msimu uliopita, hasa baada ya kufanyika kwa
mabadiliko ya dawati la ufundi katikati ya msimu, lakini wakafanya hivyo.
“Tena
ikazichapa Barcelona na kisha Bayern Munich katika fainali, timu mbili bora
kabisa katika soka la Ulaya na duniani, hivyo ningependa kuweka hai ndoto za
uipa England ubingwa wa dunia.”
Hodgson alichukua
mikoba ya kuinoa England
akijaza nafasi ya Fabio Capello Mei mwaka huu, baada ya Mtaliano huyo kushindwa
kuipa mafanikio na kuishuhudia timu yake ikiishia robo fainali ya Mataifa Ulaya
‘Euro 2012’ iliyofanyika Poland
na Ukraine .
No comments:
Post a Comment