HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 10, 2012

MIAKA 51 YA UHURU: UHURU NA MAANA YAKE KWA WATANZANIA


 Watanzania wanaosoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa Changchun, Jilin, China wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mjadala mfupi wa maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang Juma
 Mchangiaji Hamza Ibrahim akichangia kwenye mjadala mfupi wa maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili. (0696)
 Captain Mwita Vedasto Wambura akichangia kwenye mjadala wa maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili
 Captain Mwita Vedasto Wambura akichangia kwenye mjadala wa maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili

Changchun, Jilin,China

Elimu Maalum kuhusu Uzalendo inabidi itolewe ili kuwafanya watanzania waendelee kuheshimu Uhuru na dhana nzima, hayo yalisemwa na wachangiaji kwenye mjadala mfupi ulioandaliwa ili kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania hapa.

Mjadala huo mfupi, uliofanyika katika Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang jana (Jumapili), ulikuwa umeandaliwa na watanzania wanaoishi hapa, ambao wengi ni wanafunzi kwenye Vyuo Vikuu mbalimbali vilivyopo kwenye jimbo hili.

Walisema kuwa elimu ya Uraia imeonyesha mapungufu makubwa kwa kuwa haiwafanyi vijana kuwa na uzalendo kwa nchi yao, kama ilivyokuwa mwanzo.  

Walipendekeza kuwa watengenezaji wa mitaala waangalie utengenezaji wa elimu hiyo katika changamoto za uchumi wa soko huria, ambalo linapingana kwa kiasi kikubwa na dhana ya uzalendo.

Walionya kuwa hata mmomonyoko wa maadili na ubinafsi unaolisumbua taifa kwa sasa ni matokeo ya kukosekana kwa elimu hiyo ya Uzalendo. Wachangiaji Wakuu walikuwa Yazidu Saidi, Hamza Ibrahim, Captain Mwita Vedasto Wambura, Tessua Ally na Albert Memba.  Mjadala huo uliratibiwa na Innocent Mugisha.

No comments:

Post a Comment

Pages