Kocha wa zamani wa FC Barcelona, Pep Guardiola akitoka nje ya Uwanja wa Ndege jijini humo, alipotua akitokea New York Marekani anakoishim kwa ajili ya kumjulia hali mrithi wa nafasi yake na aliyekuwa msaidizi wake Tito Vilanova aliyefanyia upasuaji wa Kansa ya Tezi.
KOCHA wa
zamani wa FC Barcelona ,
Pep Guardiola juzi alilazimika kupanda ndege kutoka Marekani kurejea jijini
hapa, kwa ajili ya kumjulia hali kocha wa sasa wa klabu hiyo na msaidizi wake
wa zamani Tito Vilanova.
Guardiola
aliyeamua kupumzika majukumu katika soka akiwa nchini Marekani, alifika
hospitalini alikokuwa amelazwa Vilanova, kutokana na upasuaji wa tezi ugonjwa
uliomuanza wakati akisaidiana naye na kufanyiwa upasuaji wa dharura Novemba
mwaka jana.
Kocha huyo
ambaye anawindwa na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kwa ajili ya kukionoa
kikosi chake, ameamua kukaa pembeni ya soka hadi kiangazi kijacho ndipo anaweza
kuamua kama akubali ofa ya kufanya kazi Stamford Bridge
au la.
Upendo na
ushirikiano wake na mshirika wake huyo wa zamani ukamfanya Guardiola akate
tiketi ya ndege kutoka New York ,
anakoishi katika hekalu lake la kifahari kurejea hapa kumuona Vilanova, ambaye
aliruhusiwa kutoka hospitalini Jumamosi usiku baada ya upasuaji wa kansa ya
tezi.
Taarifa ya
kuruhusiwa kwa Villanova ilitolewa na tovuti ya klabu hiyo, wakati ujio wa
Guardiola ulishuhudiwa na wanahabari wengi akitua Uwanja wa Ndege na kisha
kupanda gari maalum kwenda hospitali, muda mfupi kabla ya kuruhusiwa.
Tovuti ya Barcelona ilisomeka: 'Kutokana
na maendeleo mazuri baada ya upasuaji, Tito Vilanova ameruhusiwa rasmi kutoka
hospitalini Jumamosi jioni. Upasuaji wa kocha huyu wa klabu yetu, ulienda vema
siku ya Alhamisi na kutakiwa kubaki hospitali kwa siku tatu.'
Wakati
Guardiola akija kumjulia hali Vilanova aliyeruhusiwa kutoka hospitalini,
wachezaji wwa Barcelona
walionesha kumuunga mkono na kumtakia heri kocha wao kwa kuvaa fualana maalum
zenye ujumbe wa heri wakati wakipasha misuli kwa pambano la Liga dhidi ya Valladolid
Jumamosi usiku.
Katika mechi
hiyo, Barcelona
iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-1, huku nyota wake Lionel Messi
akifunga moja na kumfanya amalize afikishea mabao 91 aliyofunga kwa kalenda ya
mwaka 2012, sita juu ya yaliyofungwa na Gerd Muller miaka 40 iliyopita.
Beki Mbrazil
wa klabu hiyo, Dani Alves aliutangaza ushindi huo kuwa ni maalum kwa Vilanova
akisema: 'Ushindi huu ni wa Tito. Ilitushtua na sasa imetufurahisha kuona
kwamba amerejea nyumbani kutoka hospitali. Tulikuwa hapa kumsapoti yeye kwa
kila njia tunayoweza.'
Guardiola alifanya
kazi kwa mafanikio yalityotukuka kwa kipindi cha miaka mine akiwa na Barcelona , kabla ya kuachana na jukumu hilo , huku Vilanova akijaza nafasi yake
klabuni Nou Camp.
No comments:
Post a Comment