Na Elizabeth John
MKALI wa Hip Hop Tanzania ,
Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ juzi alitambulisha ngoma yake mpya inayokwenda
kwa jina la 2030.
Roma alifanya vizuri na kibao chake cha
Mathematics ambacho alikiachia tungu mwaka jana na kinafanya vizuri hadi sasa
katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.
Akizungumzia kazi hiyo, Roma alisema
ndani yake ameelezea mambo mengi ambayo inaigusa jamii na kuwataka wapenzi wa
hip hop nchini kuisikiliza kazi hiyo ambayo anaamini ina ujumbe mzito.
“Tangu nilipoachia kazi yangu ya
Mathematics umepita mwaka mmoja na miezi kama
saba, kiukweli nimejipanga vya kutosha, kazi hii ni nzuri na nipo katika
maandalizi ya kufanya video ili kukamilisha radha kwa mashabiki wangu,” alisema
Roma.
Mbali ya kibao hicho Roma lishawahi
kutamba na vibao vyake kama Piga Magoti tusali, Tanzania na nyinginezo ambazo
zilimpa sifa na kumfanya achukue tuzo tatu za Kilimanjaro Music Awards mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment