Na Elizabeth John
BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ leo inafanya onesho
kubwa la kufunga mwaka katika viwanja vya Leades Club, jijini Dar es Salaam , likalosindikizwa
na Msondo Ngoma na vikundi sita vya burudani sanjari na bonanza kubwa la soka.
Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo, Hassani Rehani alisema
watatumia onesho hilo
kutambulisha baadhi ya nyimbo zao zitakazokuwemo katika albamu yao mpya itayozinduliwa mwakani baada ya
kukamilika.
Rehani alisema baadhi ya nyimbo zitakazotambulishwa ni
pamoja na Nyumbani ni Nyumbani, Ngumu Kumeza na Walimwengu huku wasanii kama
Ummy Wenceslaus ‘Dokii’, Haji Ramadhani, kundi la ngoma za Asili linaloitwa
Hisia na wengine watashiriki.
Onesho hilo
litaambatana na bonanza kubwa la michezo kwa timu mbalimbali za soka kuchuana
kwenye Uwanja wa Leaders huku timu ya chama cha waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA) ikicheza na Leaders Club, mechi itakayopigwa kuanzia saa nne
asubuhi.
Rehani alisema maandalizi ya bonanza na onesho hilo yamekamilika na
anaamini kuwa kuwa litakuwa na utofauti mkubwa na yaliyokwisha kufanya kutokana
na kujipanga vema kutoa burudani ya uhakika katika kuuaga mwaka wa 2012 na
kuukaribisha 2013.
Alibanisha kuwa kutokana na maandalizi ya kutosha
walioyafanya anawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo kabambe litakaloanza
na michezo kwa upande wa mpira wa miguu.
Alifafanua kuwa baada ya onesho hilo wataingia studio kukamilisha wimbo
mwingine unaoitwa Mwendapole ambao ulisuasua kurekodiwa kutokana na mtozi
kutoka Sophia record kuwa majukumu mengi ambayo yalifanya kushindikana
kurekodiwa kwa wakati.
No comments:
Post a Comment