HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2013

Aliyepooza kwa kuambiwa hana Mafao amlilia Dk. Mwinyi


Mama Joyce Mwenda (59) Akichambua Barua zipatazo 20 alizoiandikia Wizara ya Afya Ofisi ya Katibu Mkuu akidai mafao yake bila mafanikio. (Picha na Bryceson Mathias) 

Na Bryceson Mathias, Morogoro

MWANANKE aliyekuwa mfanyakazi Wizara ya Afya Joyce Mwenda (59) wa Chuo cha Wauguzi Mirembe Dodoma, na Kupooza baada ya kuambiwa na watendaji wa afya wizarani kuwa hana Mafao, amelilia Waziri Dk. Hussein Mwinyi, akimkubusha ombi lake amsaidie alipwe mafao yake.

Mwenda alijiriwa 1.11.1978 na kupunguzwa kwa waraka watumishi wa Serikali wa  2004/2005 wa kustaafishwa kwa manufaa ya umma kifungu (24) (1) cha utumishi wa umma Na.8 ya 2002 kwa barua Kumb. HEC 116/H/173 ya 29.6.2005 kwa ahadi ya kulipwa Haki zake zote.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Mwenda alisema, aliandika barua ya Malalamiko dhidi ya Ibara ya Tatu, Nne na Tano ambazo zilitambua utumishi wake kwa ahadi ya kumlipa Haki zake, kifuta jasho, na iwapo kuna upungufu wa malipo yalalamikiwe kwa muda usiopungua miezi 12, ambapo alijibiwa hana Malipo jambo lililomfanya Apooze, na alipoonana na Waziri wa Afya Dk. Mwinyi wakati wa Bunge lililopita, aliahidi kumsaidia, ndiyo maana anamlilia.

“Naomba upitie tena kukokotoa mafao yangu ili nipate stahili sahihi ninayostahili kwa utumishi wangu wa Miaka 26 na Miezi Saba”.alisema Mwenda akimtaka mwajiri amlipe akitumia mshahara wa mpya wa cheo kipya wa 118,240/= badala ya 115,640/= wa cheo cha awali.

Mwenda ambaye pia ameharibika macho, hajalipwa Pensheni yake yote (PPF) mpaka sasa tangu 2005, mapunjo, hajalipwa nauli ya familia yake ya Mume na watoto wake wanne ila nauli yake ya mtu mmoja kwenda Singida, jambo lililomsononesha na kumsababishia madhara anapolia pindi akikumbuka majibu ya kamkatisha tama kila anapokwenda.

Barua ziliyomsababishia madhira aliyonayo hadi sasa ni mbili zilizoandikwa na aliyedai ni Afisa Utumishi ikiwemo Kumb. Na HE/MP.36118/2 ya Machi 3, 2007 iliyosema…unatakiwa kutuma fomu ya maombi (Salary Area Claim Form) na kuituma ikiwa “Original na sio Photocopy”, na nyingine iliyosainiwa na Zaina Mlawa Kny y Katibu Mkuu na kumtamkia maneno makali.

Aidha mbali ya kuomba wanasheria wamsaidie, Menejimenti ya Utumishi ilimwandikia Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Kumb. C/BC 255/360/01/39 ya 22.7.10 ilyorejea barua Kumb. FC.332/349/01/130 ya 30.4.2010 iliyosema, “Malipo  ya mafao kwa mtumishi ambaye utumishi wake umekoma, yanapaswa kuandaliwa na mwajiri na kuwasilishwa wizara ya fedha ili yafanwe” ilisema sehemu yake iliyosainiwa na L. Dennis Kny ya Katibu Mkuu (Utumishi.

No comments:

Post a Comment

Pages