N Mwandishi Wetu
WAFANYABIASHARA wa soko
la Buguruni lililoko wilayani Ilala jijini Dar es Salaam wametishia kusitisha
kulipa ushuru hadi hapo soko hilo litakapoboreshwa miundombinu yake.
Akizunguza na mtandao huu, kwa niaba ya wenzake jijini jana, mmoja wa wafanyabiashara hao, Maulu
Mali alisema hawaamini kuwa serikali kuwa haina fedha ya kujenga soko hilo.
Alisema wamefikia hatua
hiyo baada ya viongozi mbambali akiwemo Rais Jakaya Kikwete kushindwa
kutekeleza ahadi zao za kujenga soko hilo.
Mali alisema hadi sasa
wamechoka kudanganywa hivyo ni vema wakasitisha kulipa ushuru hadi hapo
watakapohakikishiwa vingine tena kwa vitendo wala si kwa maneno.
Alisema hali ni mbaya
katika soko hilo haswa katika kipindi hiki cha mvua, bidhaa za wafanyabiashara
hao zinaharibika kutokana na kuvujiwa.
Alisema ndani ya soko
hilo hivi sasa kumejaa maji baada ya mifereji ya maji kuziba hali
inayohatarisha afya zao.
Alipoulizwa Ofisa
Biashara wa wilaya hiyo, Athuman Mbelwa, kuhusu tatizo linalowakabili
wafanyabiashara hao, alikirikuwa soko hilo likoa katika hali mbaya likifanana
na kiota cha ndege.
Alisema serikali iko
mbioni katika kulijenga upya soko hilo
tena kwa kiwango cha ghorofa nne, ambapo anaamini hadi kufikia mwaka 2015
litakuwa limekwisha jengwa.
“Wanajenga jingo hilo
ambalo naamini litaweza kuchukua wafanyabiashara wengi na kupunguza usumbufu
kwa wafanyabiashara katika wilaya hii”alisema Mbelwa.
Akizungumzia
wafanyabiashara wasiyorasmi alisema wanaandaa makubaliano ya pamoja
yatakayosaidia pande zote mbili katika kufanya shuhuli zao bila ya athari kati
yao.
No comments:
Post a Comment