BRISBANE, Australia
NYOTA wa tenisi raia wa Uingereza, Andy Murray, 25, kesho
Jumapili anakutana uso kwa uso na Grigor Dimitrov wa Ubelgiji katika fainali ya
michuano ya Brisbane International, huku akipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa
wa mashindano hayo.
Murray alitinga kirahisi fainali ya michuano hiyo baada ya
mpinzani wake katika mechi ya nusu fainali, Kei Nishikori kujitoa mchezoni
kutokana na kuumia goti.
Murray anayeshikilia nafasi ya tatu kidunia kwa ubora wa
tenisi na namba moja kwa Uingereza, alirudi vema kutoka mapumziko na kutoka
nyuma na kushinda 6-4 katika mechi za seti tatno mfululizo.
Mkali huyo alikuwa mbele kwa seti 2-0 katika nusu ya pili ya
pambano lao, wakati Nishikori wa Japan alipoamua kujitoa rasmi na kumruhusu
Mskochi huyo kutinga fainali.
Kesho Murray ataoneshana ubabe na mkali wa mchezo huo Dimitrov
raia wa Ubelgiji, ambaye alimshinda Marcos Baghdatis wa Cyprus kwa 6-3 5-7 7-6
(7-5) katika nusu fainali nyingine ya michuano hiyo.
Brisbane International ni michuano inayochukuliwa kama
sehemu ya maandalizi ya Murray, anayejiweka tayari kwa mashindano ya Australian
Open, yatakayofanyika kwa wiki mbili kuanzia Januri 14 hadi 27, jijini Melbourne.
No comments:
Post a Comment