LONDON, England
KOCHA Rafael Benitez amesisitiza kuwa usajili wa
mshambuliaji Demba Ba sio kamari kwa klabu yake ya Chelsea na kwamba hakuna mtu
mwenye furaha juu ya ujio Msenegal huyo kama Fernando Torres.
Torres alikuwa na msimu mbaya uliopita, wakati aliposhindwa
kuchomoza kikosini mara kwa mara mbele ya mpachika mabao mahiri Didier Drogba aliyeihama
klabu hiyo kiangazi kilichopita na kujiunga na Shanghai Shenhua.
Lakini Benitez kocha wa muda wa Blues kuelekea mwisho wa
msimu huu, amesema mambo ni tofauti kwa sasa, ambapo Torres anakaaribisha
ushindani katika nafasi yake dimbani.
Ba, 27, alimaliza usajili ulioigharimu Chelsea kitita cha
pauni milioni 7.5 akitokea Newcastle United, ambapo leo anatarajiwa kuingia
moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha matajiri hao wa jiijini hapa, katika
mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Southampton.
Na Benitez amekubali kuwa Torres atapata wasaa wa kumpumzika
katika baadhi ya mechi, kutokana na kucheza mfululizo msimu huu, ambao ameshuka
dimbani mara 31 katika kikosi cha kwanza.
Benitez alisema: “Fernando ana furaha kuona klabu inasajili
wachezaji wazuri, kwa sababu hiyo inamaanisha kwamba watashinda mechi nyingi
zaidi wakiwa pamoja.
“Nilifanya naye mazungumzo wiki chache zilizopita na alisema
kama klabu tunahitaji nyota zaidi. Sote tunatambua kuwa yeye amecheza mechi
nyingi zaidi msimu huu na hutukuweza kuwa na chaguzi nyingi zaidi katika baadhi
ya maeneo katika kikosi chetu, hasa katika ushambuliaji.
“Kwa kuondoka kwa Daniel Sturridge klabu Stamford Bridge, hiyo
inamfanya Fernando kuwa mshambuliaji mkuu wa kati ambalo kimsingi nalo ni
tatizo,” alisema Benitez.
No comments:
Post a Comment