Sir Alex Ferguson
MANCHESTER, England
Wakati Ferguson akidaiwa
kufanya vikao kadhaa na Pep Guardiola jijini New York, Marekani kwa nia ya
kumkabidhi mikoba yake kiangazi kijacho, Mskochi huyo amebainisha kuwa yu
tayari kufanya kazi kwa miaka miwili zaidi Old Trafford
KOCHA Sir Alex Ferguson yuko
katika mchakato wa kubaki kazini Old Trafford kwa miaka miwili zaidi akiinoa
klabu yake ya Manchester United.
Fergie, aliyeadhimisha miaka 71
ya kuzaliwa Siku ya Mwaka Mpya, alikuwa mwenye furaha isiyopimika akishuhudia
kikosi chake kikishinda jumla ya mabao 4-0 dhidi ya Wigan, shukrani kwa mabao
ya mawili mawili ya Robin van Persie na Javier Hernandez ‘Chicharito.’
Mskochi huyo amezidharau
taarifa kuwa anajiandaa kuachia kijiti kwa mmoja kati ya Jose Mourinho anayeinoa
Real Madrid, au kocha wa zamani wa FC Barcelona, Pep Guardiola kiangazi kijacho.
Ferguson alisema: “Nina
matumaini ya kubaki kazini Old Trafford kwa kipindi kidogo kijacho. Hakuna haja
ya kugeuza hilo mjadala, naweza kukuhakikishia hivyo.
“Unaweza kuzungumza kuhusu
mmoja wa mameneja vijana wenye kusisimua – kuwa yeye anaweza kuja kufanya kazi
hapa katika kipindi cha miaka miwili?
“Nadhani mameneja wa daraja la
juu daina huwa katika mahitaji.
“Guardiola, Mourinho, David
Moyes, kuna mameneja wengi tu nje ya hapa ambao wana mafanikio makubwa dimbani
na mimi kamwe sijui mipango yao.
“Nani ambaye anajua wapi
watakuwa makocha hao katika kipindi miaka miwili au mitatu ijayo,” alisisitiza
Fergie, akiwa na furaha ya ushindi dhidi ya Wigan.
Akiuzungumzia ushindi huo,
Fergie alisema: “Ulikuwa ni mwanzo mzuri wa mwaka 2013. Tuko juu kwa tofauti ya
pointi saba, tukiongoza ligi, huku kukiwa kumebaki mechi 17 msimu kufikia
tamati.”
No comments:
Post a Comment