DAR ES SALAAM, Tanzania
JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam inawashikilia Polisi watano kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa sh. mil 150, tukio lililotokea Desemba 14
mwaka jana katika eneo la Kariakoo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
esSalaam Jana Kamanda Kova, alisema alichounda yeye kwa wakati huo ni jopo la
uchunguzi ambalo taarifa zake hazina ulazima wa kutolewa mbele ya jamii zaidi
ya kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa kile walichokibaini.
“Naomba mnielewe leo nimekuja na kile nilichorekodi
wakati ule na mtasikiliza ila ninachoweza kuwaambia jopo halipewi hadidu za
rejea na linaundwa na wataalam, tofauti na tume ambayyo hupewa hadidu za kitu
wanachotakiwa kufanya na kisha majibu yake kupelekwa kwa jamii”alisema Kova.
Aliongeza kuwa baada ya kuunda jopo kwa wakati huo
jukumu la kupeleleza sakata la Dk Ulimboka liliondoka mikononi mwake na kuwa
chini ya ofisi ya mkurugenzi wa makosa
ya jinai nchini(DCI) na kwamba kama kutakuwa na mswali yenye kumuhusu Dk
Ulimboka ni vema waandishi wakawasiliana na ofisi ya Mkurugenzi huyo
Katika video hiyo inayoonyesha imefanyiwa marekebisho
(Editing), Kamanda Kova anaonekana akiwa na askari wawili, mmoja akiwa na nyota
tatu huku kukiwa na kinasa sauti cha kituo cha Televisheni ya ITV peke yake katika eneo la kuwekea vinasa
sauti.
Akizungumzia tukio la ujambazi lililotokea eneo la
Kariakoo Desemba 14 mwaka jana Kova alisema, baada ya tukio hilo kulikuwa na
taarifa kuwa askari waliopambana na majambazi walitoweka na mfuko wa fedha,
hali iliyosababisha jeshi hilo kanda maalum kuunda jopo ya kuchunguza suala
hilo.
Alisema dalili za awali zinaonesha kuwepo kwa hali ya
ushiriki wa askari watano katika upotevu wa fedha hizo na kwamba askari hao
wanashikiliwa huku uchunguzi zaidi ukifanyika.
Aliongeza kuwa askari wanaoshikiliwa ni wenye vyeo
vya steshen staf sajent mmoja na wengine wannne wenye veo vya ukoplo.
Alisema askari hao kwa sasa watajibu mashtaka ya
kijeshi kabla ya kufikishwa katika mahakma za kiraia.
Aidha Kamanda Kova, alisema mbali na askari hao pia
wanawashikilia watu wengine wawili kuhudiana na tukio hilo ambapo aliwataja
kuwa ni Deogratias Kimaro (30), mkazi wa Karakata na Kulwa Mwakabala (30),
mkazi wa KijiweSamli
Wakati huo huo Kamanda Kova leo amelazimika kutumia ushahidi wa video, kukanusha kauli iliyowahi kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini, kuwa aliunda tume katika sakata zima la kuchunguza utekwaji wa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Dk Stephen Ulimboka.
Mbali na kutumia video kukanusha suala hilo pia Kamanda kova aliomba suala lolote linalohusiana na Dk Ulimboka asiulizwe yeye kwa sasa kwa kuwa jukumu hilo limeshaondoka katika uwezo wake wa kazi na lipo kwa wakubwa wake kiofisi
No comments:
Post a Comment