DAR ES SALAAM, Tanzania
MWANASIA
mkongwe nchini Senator Julius Miselya amesema hatarajii kupatika Katiba Mpya
itakayolingana na matakwa ya wengi, kutokana maoni ya wananchi bila kuwepo
rasimu ya kuwaongoza.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni Miselya ambaye pia ni mwaasisi wa Chama
Demokrasia (DP), siyo Mchungaji Christopher Mtikila kama inavyodhaniwa na
wengi, alisema kinachofanyika hivi sasa ni kiini macho na kupoteza muda wa
wananchi.
Alisema
walichotakiwa kukifanya watawala ni kuandaliwa rasimu yenye mapendekezo kisha
kuisambaza kwa wananchi, ambapo baada ya kuipitia ndipo wapendekeze kipi
kiingizwe kwenye Katiba hiyo mpya.
Miselya
alisema kwa utaratibu unaotumika wa kutoa maoni haoni kama una nguvu ya
kubadili kile kinacholalamikiwa bali anaamini makusudio yatabaki yale yale ya
kulinda serikali ya chama kilekile kilichoifikisha nchi hapa ilipo.
Aidha,
hali hiyo ya kukosekana rasimu hiyo
inachangia wananchi kushindwa kabisa kutoa maoni yenye tija na badala yake kila
mtu anajisemea kile anachokitaka binafsi.
“Kinacho
nisikitisha hapa ni wananchi kuchangia maoni huku wakiwa hawajui hata katiba
yetu ya zamani ina upungufu gani au ina
mazuri yepi, hili ni jambo litatuweka pabaya katika kupata maoni yenye ya
msingi, ndiyo maana tunasikia baadhi ya wanawake wakitoa maoni ya kutaka waolewe na wanaume
wawili”alisema Miselya.
Miselya
alisema hadi sasa ukiangalia maoni yanayotolewa yamekuwa hayalengi kulisaidia
taifa hili, mwisho wake watawala watakutana wenyewe na kupitisha matakwa yao.
“
Mimi naona katiba itakayopatikana haitakuwa na mabadiliko bali itakuwa ile ile
ya kulinda maslahi ya watu wachache kama ilivyo sasa”alisema Miselya.
Alisema
kinachojitokeza hivi sasa ni Tume hiyo
ya mabadiliko ya Katiba kufujaji wa fedha nyingi zinazotokana na kodi za walala
hoi kwa kitu ambacho matokeo yake yanafhamika.
No comments:
Post a Comment