MKALI wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Khalid Mohammed ‘TID Mnyama’ anajipanga kuachia albamu yake ya tatu
inayokwenda kwa jina la ‘Kiuno’.
TID alishawahi kutamba na albamu
zake mbili ikiwemo ya ‘Nyota yangu’ ambayo ilifanya vizuri na kumtangaza katika
nchi za jirani.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam, TID alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi
hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri kutokana na nyimbo zote zilizokuwepo humo
kufanya vizuri katika soko hilo.
Alisema anawaomba mashabiki wa kazi
zake wakae mkao wa kula kwaajili kuipokea kazi hiyo ambayo imetengenezwa kwa
kufuata maadili ya Mtanzania.
“Nafurahi kwasababu kazi zangu
zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu naomba mashabiki wangu msichoke
kunisiliza kwani bado kuna vitu vizuri ambavyo nawaanndalia,” alisema TID.
Mbali na kibao chake cha Kiuno
ambacho kinabeba jiana la albamu hiyo, TID alishawahi kutamba na kibao chake
cha ‘Nyota yangu’ ambacho kilimtambulisha na kufanya vizuri zaidi licha ya kuwa
na vibao vingi.
No comments:
Post a Comment