Na Elizabeth John
BONDIA Fadhil Awadhi ‘Mnyama Chui’
amefanikiwa kukata ngebe za Yohana Mathayo ‘Tembo mtoto’ kwa kumtwanga kwa KO
katika raundi ya nne ya mchezo huo uliofanyika katika ukumbi wa Texas Manzese jijini
Dar es Salaaam.
Mchezo huo ulifanyika juzi ulikuwa
na upinzani mkubwa ulianza kwa kila mmoja kucheza kwa kujihami huku Tembo Mtoto
alikuwa akirusha makonde mazito kwa kushtukiza lakini umahiri wa Mnyama Chui
ulifanya kuhimili mikikimkiki hiyo.
Mnyama Chui aliweza kuhimili
makonde hayo mazito lakini muda mwingi alionekana kumkabili vema mpinzani wake
kwa kumrushia makonde yaliyofanya katika raundi ya nne Tembo Mtoto kunyanyua
mikono juu kuashiria kusitisha kuendelea na pambano hilo.
Mwamuzi wa pambano hilo, Emmanuel
Mlundwa baada ya kuona Tembo Mtoto kusalimu amri alimtangaza Mnyama Chui kuwa
mshindi wa poambano hili lililokuwa na upinzani wa aina yake hali iliyofanya
kuvuta hisia za wadau wengi wa mchezo huo Mkoa wa Dar es Salaam.
Pambano hilo lililokuwa chini ya
usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) lilitanguliwa
na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Adam Yahya alimpiga kwa tabu Good
Silver kwa point 39 kwa 37.
Rashid Chidox alimkata ngebe Bonny
Gude kwa KO katika raundi ya pili, Habibu Pengo alitandikwa na Roja Zengo
kwa KO kwenye raundi ya kwanza, Fabian Lymo ‘Lampard’ alimkung’uta Hassan
Mmanga kwa KO katika raundi ya tatu.
No comments:
Post a Comment