Kikosi Bora cha Mwaka 2012 ‘FIFA/FIFPro
World XI,’ kutoka kushoto waliosimama nyuma ni Ronaldo, Marcelo, Ramos, Pique,
Alves, Casillas, wakati waliosimama mbele ni Falcao, Messi, Iniesta, Xavi na
Alonso. Kikosi hicho kilitangzwa juzi usiku wakati wa hafla ya kumtunukia
Mwanasoka Bora wa Mwaka ‘Ballon D’Or’ iliyonyakuliwa na Lionel Messi.
LONDON, England
Wakali wanaounda kikosi
hicho ni: Iker Casillas, Dani Alves, Gerard Pique, Sergio Ramos, Marcelo, Xabi
Alonso, Xavi Hernandez, Andres Iniesta, Cristiano Ronaldo, Radamel Falcao na
Lionel Messi
BEKI wa kimataifa wa England, Ashley
Cole amelipiga kijembe Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa kusema
anahitaji kuwa na pasi ya kusafiria ya Hispania, ili aweze kutambuliwa kuwa ni
beki bora wa kushoto duniani kwa sasa.
Kauli ya mshindi huyo wa taji
la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, umetokana na kutoingia kwake yeye ama
nyota yeyote wa Chelsea katika Kikosi Bora cha
Mwaka ‘FIFPro World XI 2012’ kilichotangzwa juzi huko Zurich, Uswisi.
Kama hiyo haitoshi, Ligi Kuu
ya England haikutoa mchezaji
hata mmoja miongoni mwa wakali 11 waliotangazwa kuwamo kikosini, huku wote
wakitoka katika Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ – 10 kati yao
wakitoka klabu za Real Madrid na Barcelona.
Sita miongoni mwa nyota hao 11
wanaounda kikosi hicho bora wakiwa ni walioiwezesha Hispania kutwaa ubingwa wa
Mataifa Ulaya Euro 2012.
Wachezaji walioingia katika
kikosi hicho ni: Iker Casillas, Dani Alves, Gerard Pique, Sergio Ramos,
Marcelo, Xabi Alonso, Xavi Hernandez, Andres Iniesta, Cristiano Ronaldo,
Radamel Falcao na Lionel Messi.
Katika mjadala mpana kupitia
mtandao wa kijamii wa Twitter, mshambuliaji wa Barnet, Steve Kabba alikosoa
kutokuwapo kwa Cole kikosini, lakini nyota huyo wa England akajibu: “Hakuna utani
kinachotokea hapa kinashangaza. #Nahitaji pasi ya kusafiria ya Hispania.”
Mchangiaji mwingine na nyota
wa zamani Stamford Bridge, nguli Ron ‘Chopper’ Harris alisema: “Inashangaza
sana kuona timu
iliyotwaa ubingwa wa Ulaya haijaingiza mchezaji hata mmoja katika kikosi bora
cha mwaka cha Fifa.
“Achana na mfumo huo
uliotumika – kama nitaambiwa nichague kati ya Marcelo
na Ashley Cole, sitomchagua Marcelo. Lakini pia kuna mameneja bora Ulaya, akiwamo
Jose Mourinho!”
Mzozo wa ubaguzi baina ya John
Tery na Anthon Ferdinand, ulimsukuma beki wa Manchester United, Rio Ferdinand kutomuunga
mkono Cole kuwamo kikosini, baada ya nyota huyo ‘mweusi’ kumtetea Terry katika
sakata hilo.
Badala yake Ferdinand akachangia
kwa kushangaa kutoingia hapo kwa mshambuliaji wa Manchester United, Robin van
Persie, aliyekuwa akichezea Arsenal. Akaandika: “Kwa vipi Van Persie hayumo
katika kikosi hicho?”
Nyota wa zamani wa timu ya
taifa ya Ujerumani, Lothar Matthaus alichangia kwa kuandika: “Sielewi kama hiki
kikosi cha FIFPro World XI, kinatakiwa kuhusisha nyota wa La Liga tu.”
Harris naye akaongeza: “Watu
wengi duniani wanasema Ligi Kuu ya Hispania ni bora zaidi duniani. Lakini kama
ukiziweka kando Barcelona
na Real Madrid, kipi kingine kilichomo humo?”
Miongoni mwa wakosoaji wa
kikosi hicho walishangazwa na kutowamo kikosini kwa kiungo wa kimataifa wa
Italia, Andrea Pirlo, kiungo mahiri aliyefanya mambo makubwa na kuiwezesha Juventus
kutwaa Serie A na kuifikisha Azzurri fainali ya Euro 2012.
No comments:
Post a Comment