Boateng wa pili kulia akiwa na Mathiue Flamini wakiondoka dimbani baada ya kubaguliwa na mashabiki, huku wakiombwa kutofanya hivyo na wachezaji wa Pro Patria.
MILAN, Italia
"Nilimuita kidogo Kevin-Prince Boateng wakati
akiondoka dimbani na nikampongeza sana kwa majibu yake dhidi ya ubaguzi wa
rangi ambayo ni fedheha iliyochukua nafasi huko Busto Arsizio. Nina furaha sana
kwa aina hii ya majibu iliyotoa Milan kwa wabaguzi"
MMILIKI wa AC Milan, Silvio Berlusconi – ambaye pia ni
Waziri Mkuu wa zamani wa Italia, alimsifia Kevin-Prince Boateng kwa msimamo
alioonesha wa kuongoza wenzake kususia mechi kama ishara ya kukerwa vitendo vya
ubaguzi wa rangi.
Boateng aliongoza wachezaji wa Milan ‘Rosonerri’ kuondoka
uwanjani na kuvunja pambano, baada ya kufanyiwa ubaguzi wa rangi wakati wa
mechi yao ya kirafiki na klabu ya madaraja ya chini ya Pro Patria.
Berlusconi, asisitiza kuwa klabu yake itaendelea kuchuakua
uamuzi huo katika mechi zake pindi vitendo vya ubaguzi vitakapofanywa na
mashabiki ama wachezaji, zikiwamo mechi za michuano ya klabu barani Ulaya.
"Nilimuita kidogo Kevin-Prince Boateng wakati akiondoka
dimbani na nikampongeza sana kwa majibu yake dhidi ya ubaguzi wa rangi ambayo
ni fedheha iliyochukua nafasi huko Busto Arsizio.
"Nina furaha sana kwa aina ya majibu iliyotoa Milan
kutokana na kilichotokea na nina kuhakikishia mahali popote sisi
tutakapofanyiwa hivyo, Milan itasusia mechi na kuondoka uwanjani."
Aidha, Boateng amesisitiza kuwa, yu tayari kususia na
kuondoka dimbani tena katika mechi yoyote kama atashuhudia akifanyiwa vitendo
vya ubaguzi wa rangi na mashabiki wa mchezo huo.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha Cable News Network (CNN), Boateng, 25, alisema: "Sitojali kama ni
mchezo wa kirafiki, Ligi Kuu na michuano mingine nchini Italia, au Ligi ya
Mabingwa Ulaya – nitasusia mechi na kuondoka uwanjani tena."
Hata hivyo, Gordon Taylor, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa
Chama cha Wanasoka wa Kulipwa, ameonya kuwa wachezaji wanaweza kujikuta
matatizoni kama watasusia mechi pindi wanapofanyiwa vitendo vya ubaguzi katika
mechi nchini hapa.
"Ubaguzi wa rangi lazima uripotiwe kwa maofisa wa
mchezo na wachezaji kupitia manahodha wao. Kama vitendo hivyo vitaendelea,
maofisa wa mechi ndio wataamua kutoendelea na mechi," alisisitiza Taylor.
Tayari Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na Shirikisho
la Soka barani Ulaya (Uefa), bodi zenye mamlaka ya juu duniani na Ulaya
zilishakataza kuhusu wachezaji kususia mechi na kuondoka dimbani pindi
wanapobaguliwa.
No comments:
Post a Comment