LONDON, England
KOCHA wa Chelsea, Rafael Benitez, ametetea uamuzi wake wa
kubadili kikosi kilichokwaana na QPR katika mechi ya juzi iliyoisha kwa timu
yake kulimwa bao 1-0.
Kwa kipigo hicho kutoka kwa timu inayoburuza mkia kwenye
msimamo wa Ligi Kuu ya England, kocha huyo amejikuta katikati ya lawama kwa
kupanga kikosi dhaifu.
Kikisi cha juzi kilikuwa ni tofauti na kile kilichocheza na Everton
mwishoni mwawiki na kushinda mabao 2-1.
Nyota ambao hawakucheza mechi ya mwishoni mwa wiki na
kupangwa katika mechi ya juzi, ni Ryan Bertrand, Marko Marin, Victor Moses, Oscar na Ross Turnbull.
Hata hivyo, Benitez ametetea uamuzi wake kwa kusema ni
vigumu kuchezesha kikosi kimoja kwa kipindi chote cha krismas na mwaka mpya.
Alisema alichofanya katika mechi hiyo ni kuwapa nafasi
wengine na kuwapumzisha wengine kama Juan Mata na Eden Hazard.
"Tumecheza vizuri tena kwa kujiamini, alisema Benitez na kuongeza: "Tulibadili baadhi ya
wachezaji, lakini ni Marko Marin ndiye pekee ambaye amekuwa hachezi mara kwa
mara.
Katika mechi ya mwisho (dhidi ya Everton), Moses alicheza
kama ilivyo kwa Oscar.
"QPR wao walicheza kwa kuvizia na kupiga pasi fupifupi.
Hii ndio ilikuwa tofauti kubwa kati yetu na wao hasa kuelekea mwishoni mwa
mechi.
"Huwezi kuchezesha kikosi kimoja kila mechi. Unapocheza
ugenini na timu inayoburuza mkia, unapaswa kuwaamini wachezaji ako, nami
nawaamini,” alisema Benitez katika hali ya kutetea kipigo hicho.
Kwa kipigo hicho, Chelsea imebaki nafasi ya nne kwenye
msimamo ikiwa na pointi 38, ikitanguliwa na Man Utd 52 na Mam City(45) na Tottenham yenye pointi 39.
Tangu Benitez atwae mikocha ya timu hiyo kutoka kwa Roberto
Di Matteo, amekuwa hapati sapoti kubwa
ya mashabiki wa timu hiyo, hivyo kipigo cha juzi kimeibua mengi.
Bao lililowapa wenyeji pointi tatu, lilifungwa dakika ya 78 na
Shaun Wright-Phillips, ukiwa ni ushindi wa pili kwa timu hiyo katika msimu huu.
Wakati Chelsea wakipata kichapo, Liverpool wakicheza
nyumbani walivuna ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sunderland.
Mabao mawili ya Liverpool yalifungwa na nyota wa kimataifa
wa Uruguay, Luis Suarez, baada ya kinda Raheem
Sterling kuifungia la kwanza dakika ya 19.
Suarez sasa amefikisha mabao 15, akiwa nyuma kwa bao moja
dhidi ya kinara Robin van Persie wa Manchester United.
Liverpoo sasa wamefikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi
21, hivyo kuwa nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment