NEW YORK, Marekani
MCHEZAJI Venus Williams anaamini ameiva tayari kwa kuonesha
kiwango katika michuano ya mwezi huu ya Australian Open, baada ya kufanya vema
bila kichapo katika michuano ya nyota mmoja mmoja ya Kombe la Hopman.
Williams alikuwa na michuano ya aina yake ya Kombe la
Hopman, alikomshinda Mhispania Anabel Medina Garrigues kwa seti mfululizo
Alhamisi kukamilisha mechi tatu za nyota mmoja mmoja alizocheza.
Lakini Mmarekani huyo anaamini kuwa kutwaa ubingwa wa Hopman
kutamsukuma kupata mafanikio, michuano ambayo nyota mwenzake wa timu ya taifa John
Isner alijitoa katika michuano hiyo mapema katika siku ya kwanza kwa matatizo
ya goti.
Nyota huyo mwenye miaka 32, alikuwa na matumaini ya kupata
mechi moja ya mchezaji mmoja mmoja Jumamosi, kabla ya kupaa zake jijini Melbourne
kupigania kutwaa Grand Slam ya kwanza kwa mwaka huu wa 2013, katika michuano
itakayoanza Januari 14.
Williams, ambaye hajawahi kuvuka raundi ya nne katika
kuwania Grand Slam, tangu alipofanya hivyo mwaka 2010 kwenye US Open, ameonekana
kuimarika kiwango kama alivyoonekana katika Kombe la Hopman.
No comments:
Post a Comment