HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 09, 2013

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZINDUA BARABARA YA MFENESINI-BUMBWINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati), Mwakilishi wa ADB Tanzania, Toniya Kandiero, Naibu Waziri wa Mindombinu na Mawasiliano, Issa Haji Gavu, Katibu Mkuu wa Miundombinu ,Mawasiliano,Dk.Juma Malik  Akili, na Mkuu wa Mkoa wa Kasakazini Unguja Pembe Juma (kushoto), wakitembea katika Barabara ya Mfenesini-Bumbwini baada ya kufunguliwa Rasmi jana, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana. Barabara hiyo imejenga na Kampuni ya Mecco kwa umefadhili wa na Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi, ikiwa ni shamrashamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Shein, akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja.
Dk.Ali Mohamed Shein na Mwakilishi wa ADB Tanzania, Toniya Kandiero,wakikata utepe kufungua Barabara ya Mfenesini-Bumbwini, iliyojengwa na Kampuni ya Mecco kwa  ufadhili wa Benki ya Dunia  kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, wakimsikiliza Dk. Shein, alipokuwa akizungumza nao katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja.

No comments:

Post a Comment

Pages